Utoaji matone ya vitamini A kwa watoto walio umri wa miezi sita hadi miaka mitano.
Afisa Mtafiti wa Sayansi ya Chakula na Lishe Wessy Meghji akionesha aina ya vyakula ambavyo vinaongeza vitamini A, kushoto ni Elifatio Towo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe |
TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA
PROGRAM YA UTOAJI MATONE YA VITAMINI A KWA WATOTO WALIO KATIKA UMRI WA MIEZI 6 HADI MIAKA MITANO
Upungufu
wa vitamini na madini ni mojawapo ya matatizo makubwa ya kilishe
yanayowaathiri hasa watoto na wanawake walio katika umri wa kuzaa hapa
Tanzania. Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii
(Demographic and Health Survey) za mwaka 2010 zinaonesha kuwa hapa
Tanzania upungufu wa vitamini A unaathiri asilimia 33 au theluthi moja
ya watoto walio chini ya miaka mitano na asilimia 37 au zaidi ya
theluthi moja ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Upungufu
wa madini chuma unaathiri asilimia 59 au zaidi ya nusu ya watoto wadogo
na karibu asilimia 41 au karibu ya nusu ya akina mama wajawazito, na
pia upungufu wa madini joto unakadiriwa kuathiri asilimia 7 ya
Watanzania. Njia mojawapo ambayo inatumika kupunguza tatizo
No comments:
Post a Comment