Header Ads

KINANA AZURU KUIJULIA HALI FAMILIA YA MAREHEMU DK. MGIMWA, KALENGA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akisalimiana na mama mzazi wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dk. William Mgimwa, Bibi Consolata Mgovano (wa pili kulia), dada wa marehemu, Stanisla Mgimwa (kulia), pamoja na mtoto wa marehemu, Johakim Mgimwa alipokwenda kuwajulia hali nyumbani kwao Magunga, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini leo. Kinana aliamua kwenda kuwajulia hali tena baada ya mwanzoni kushiriki mazishi ya marehemu Dk. Mgimwa mwezi uliopita.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 Kinana akijadiliana jambo na familia hiyo ya marehemu Dk Mgimwa.
 Johakim Mgimwa akitoa shukurani kwa Katibu Mkuu  wa CCM, Kinana kwa moyo wake wa huruma kwa kwenda tena kwa mara pili kuwajulia hali kijijini hapo.
 Kinana akiondoka  mara baada ya kuagana na familia hiyo leo
 Kinana akivishwa skafu na kijana wa chama hicho, alipowasili Kata ya Ifunda, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini ambapo alifanya mkutano wa ndani na wajumbe wa wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Ifunda leo, akitokea mkoani Mbeya kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho.
 Kinana akisalimiana na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata hiyo baada ya kuwasili leo mchana.
 Kikundi cha kwaya cha Ngama kikitumbuiza kwa nyimbo za CCM wakati wa mkutano huo
 Mmoja wa akina mama wafuasi wa CCM akishangilia huku akipeperusha  kipeperushi chenye picha ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Ifunda Mjini leo.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Damas Masonda akitumbuiza kwa wimbo wa kuisifu CCM wakati wa mkutano huo wa hadhara.
 Msanii Catherine Oseah akiimba kwa hisia wimbo wa CCM wakati wa mkutano huo
Wafuasi wa CCM wakishangilia wakati Kinana akihutubia katika mkutano huo

No comments:

Powered by Blogger.