TAMASHA LA KRISIMASI LAFANA UWANJA WA TAIFA,SOLLY MAHLANGU WA AFRIKA KUSINI AWAKUNA VILIVYO WATAZAMAJI
Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akizungumza mbele ya watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.Lukuvi amewataka watazamaji na washabiki wa tamasha hilo na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwa amani,upendo na utulivu,ameongeza kuwa pia Serikali itahakikisha usalama upo na wa kutosha kwa watu wake,pichani kati ni Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha hilo Bwa.Alex Msama.

Mmoja wa wageni waalikwa katika tamasha la Krisimasi,Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pichani kati akiwatakia heri na fanaka Watazamaji na Watazania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya. 

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Zambia,Epraim Sekereti akiimba jukwaani kwenye tamasha la krismasi jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mh.Lukuvi.
Baadhi ya Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka kikundi cha Living Waters wakitumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini dar.
Baadhi ya waimbaji waliombatana na mwanamuziki nyota kutoka nchini Afrika Kusini Solly Mahlangu,wakimpa back up mkali huyo wa injili.
Baadhi ya Wapiga vyombo wa mwanamuziki Solly Mahlangu wakiwajibika jukwaani.
Baadhi ya mashabiki wa Mwanamuziki Solly Mahlangu kutoka nchini Afrika kusini wakifurahia
Pichani juu na chini ni Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu akiwaimbisha mashabiki wake jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini dar.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo.
Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili Upendo Nkone akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo mbele ya mashabiki kibao (hawapo pichani) wakati wa tamasha la krisimasi likiendelea jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini Dar.
Pichani shoto ni Mwimbaji nyota wa muziki wa injili,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima,wakishambulia kwa namna ya pekee kabisa,huku miluzi na shangwe za watazamaji zikivuma kila kona ya uwanja,jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi.
Rose Muhando akiimba wimbo wake wa Utamu kwa Yesu mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani) jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambako tamasha la Krisimasi likiendelea jioni ya leo.
Muimbaji wa nyimbo za kuabudu,Upendo Kilahiro akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi,linaloendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.
Baadi ya Waimbaji wa kundi la Glorious wakiimba jukwaani
Mwimbaji wa nyimbo za injili,Boni Mwaitege pichani kati na madansa wake wakiwaimbisha mashabiki wao jioni ya leo .
Sehemu ya umati wa Watu wakifuatilia tamasha la Krisimasi,linalofanyika jioni ya leo ndani ya Uwanja wa Taifa,ambalo limejumuisha wanamuziki mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Kundi la waimbaji mahiri wa muziki wa injili The Voice wakiimba Acapera zao jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi linalofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na kampuni ya Msama Promotions Ltd
Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akiwasalimia mashabiki watazamaji mbalimbali waliofika kwenye tamasha hilo,linalofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar .
No comments:
Post a Comment