MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA
Mtangazaji wa kipindi cha mboni show Mboni Masimba akimkabidhi zawadi mtoto yatima Ally Mustapha baada ya kuimba vizuri katika mlo uliandaliwa na Mboni katika ukumbi wa Highland hall
baadhi ya watoto yatima wakiwa katika ukumbi wa highland hall na mc wa shughuli hiyo Mc Zipompampa akiwa na mtoto Ally Mustapha. (Picha Zote na Denis Mlowe).
Wageni rasmi katika hafla maalum ya mlo wa pamoja uliondaliwa na kipindi cha Mboni Show, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi (kulia), Mboni Masimba katikati akiwa na mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Asas Abri, mgeni kutoka Nigeria.
======= ====== =======
MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA
Na Denis Mlowe,Iringa.
MTANGAZAJI wa kipindi cha ‘Mboni Show’ kinachorushwa na luninga ya EATV,Mboni Masimba leo amejumuika pamoja katika hafla na watoto yatima zaidi ya 200 walioko katika mkoa wa Iringa.
Katika hafla hiyo umejumuisha vituo vitatu vya watoto yatima vilivyoko mkoani Iringa vya Upendo center na Tosamaganga na kingine kilichoko katika wilaya ya Mufindi cha Moyo kwa Moyo.
Hafla hiyo ya kula chakula cha mchana na yatima imefanyika katika ukumbi wa Highland hall na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara maarufu mkoani hapa akiwemo mkurugenzi wa makampuni ya Asas, Salim Abri Asas na mgeni rasmi alikuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi..
Mbali ya kuwalisha watoto hao mboni ametumia muda huwa kuendesha kipindi chake cha Mboni Show kwaa kujumuika na watoto hao.
No comments:
Post a Comment