THAILAND YAMSHITAKI RASMI WAZIRI MKUU WAKE ‘YINGLUCK SHINAWATRA’ KWA TUHUMA ZA UFISADI
Tume ya kupambana na ufisadi nchini Thailand imemshitaki rasmi waziri mkuu aliyeondolewa madarakani Yingluck Shinawatra kwa madai ya kupuuza jukumu lake katika usimamizi wa mpango uliokosolewa vikali wa kutoa ruzuku ya mchele.
Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama ya katiba kumuondoa
madarakani waziri mkuu huyo ambaye anatuhumiwa kwa kuruhusu mpango huo
wa mchele uliokuwa sera muhimu katika utawala wake kuendelea licha ya
kushauriwa kwamba ulikuwa ukitumiwa vibaya na kuzongwa na ufisadi.
Uamuzi huo unamaana kuwa mwanamama YingLuck atakabiliwa na
kura ya kumng’oa madarakani katika baraza la seneti ikiwa theluthi tano
ya kura zitaunga mkono uamuzi wa kumtia hatiani na anaweza kuzuiwa
kushiriki katika masuala ya siasa kwa miaka mitano.
No comments:
Post a Comment