Header Ads

PICHA RASMI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS-IKULU:MAKAMU WA RAIS DKT.GHARIB BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU FROSSIE CHIYAONGA BALOZI WA MALAWI NCHINI TANZANIA ALIYEFARIKI GHAFLA IJUMAA WIKI ILIYOPITA

  Marehemu, Balozi Frossie Chiyaonga, enzi za uhai wake.
  Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili huo unatarajia kusafirishwa kuelekea Malawi kwa maziko.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Frossie Chiyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji baadhi ya wanandugu na familia ya aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa salamu za rambirambi, wakati wa shughuli hiyo.
  Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.

No comments:

Powered by Blogger.