Header Ads

Mashairi ya wimbo wa Diamond Platnumz - Sikomi Lyrics

Verse I
Wanasemanga Mapenzi safari,Unavyopita ndo jinsi Unajongea,
Ila niendako ni mbali sijui ka ntafika sababu natembea,
Niliposikia habari yakisifika Nkakesha nangojeaa.
Akabariki jalali na nikawika muziki nikauotea,
Ile kumpaka makaa nikadhania ndio bongo movie,
kumbe mapenzi hayataki haraka ni tango natia tu chumvi,
Mwenzenyu nikaoza haswa,na kujitia kitandani mjuzi,
Eti nataka fukuza paka badala ya Mbwa nikafuga mbuzi..
.mmmh wivu kanifanya nikagombana na marafiki.
Ugomvi na mamangu akiniambia siambiliki.
Moyo Ukaniambia,Naseeb sasa mapenzi basi
ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi.
Esma ananambia mdogo wangu mapenzi wangu
Basi ila nang'ang'ania nikiumizwa na huyu kesho na mwengine oh mbona sikomi... Sikomi,sikomi,licha ya mateso haya..

Chorus
Najiuliza oh sikomi,oh sikomi,
mbona(sikomi) mbona jamani,
sikomi licha ya mateso haya ah!...

Verse II
 Mmmh! Aliyonifanyia wa central, akia-Mungu siyawezi sema ila nimejifunza kesho siwaamini wacheza sinema;Moyo walinipatia mateso,siwezi kumeza siwezi tema..
 ,Maana sikushangaa ile ghafla toka CCM kwenda Chadema.
Wanasema kitanda ukitandika sharti ukilalie,
Nikajitia ukamanda yatakwisha wacha nivumilie,
 kila Giza kikitanda ndo visa majozi mi nilie .
penzi yakatia parapanda kuwaita waje washambulie,
aaah acha na penny we darling,nilomuhongaga gari
 aliponiambia ana mimba na mwisho wa siku akaichomoa chali!!,
 Mola akanitunuku Zari,akanizalia dume na mwali nilivyomjinga
 Nika-cheat aibu mpaka kwa vyombo vya habari.
 Moyo unanambia Naseeb sasa Mapenzi
Basi ila nang'ang'ania najaribu kuipinga nafsi...
Laizer ananambia Simba mapenzi basi ila nang'ang'ania
nikiumizwa na huyu kesho na mwengine...

Chorus
 Oh! mbona sikomi(Mboona)...sikomi (Mboona)..
Jamani sikomi. Licha ya mateso haya, Nishafumaniwa,

oh sikomi Nikafumaniwa Mimi,sikomi.
 Nishapambana na watu (Sikomi) Licha ya mateso haya! (mateso mama)

No comments:

Powered by Blogger.