Header Ads

UMUHIMU WA MAZINGIRA

              UMUHIMU WA MAZINGIRA
Mazingira ni sehemu inayomzunguka binadamu pamoja na viumbe hai wote.MAZINGIRA NI MUHIMU KWA BINADAMU NA BINADAMU NI MUHIMU KWA MAZINGIRA.Kwa hiyo vyote vinategemeana,kwa hiyo binadamu yoyote duniani anatakiwa kuyapenda mazingira yake yanayo mzunguka kwa kuyafanyia usafi mfano kufagia,kufyeka,na hata kuyatunza kwa kiwango kinachotakiwa
    Tumeona  serikali  imejitahidi sana kutoa elimu kwa wananchi kuyatunza mazingira na kuyapenda serikali imejitahidi hata kutumia vikundi vya sanaa kuhamasisha madhara yatokanayo na kutotunza mazingira tumeona raisi wetu mpendwa jakaya mrisho kikwete akitumia kauli maralia haikubariki akimaanisha kama tutayatunza mazingira yetu kwa kudhibiti mbu wanaozaliana kwenye taka chafu au madimbwi au kufyeka nyasi zinazo sababisha kuongezeka kwa mbu  pia magonjwa mbalimbali kama ya tumbo na kipindu pindu hutokana na mazingira machafu ambayo wananchi hawayapi umuhimu kwa kuyatunza pia kumwaga maji ovyo kwenye mazingira ambayo haya stahili.nashukuru viongozi wote duniani kwa kuhamasisha nchi zao kwa kujali na kuona umuhimu wa mazingira .Taifa lolote duniani lisilo jail umuhimu wa mazingira ya nchi yaobasi itakuwa ni taifa lisilo na taswira nzuri.Nwashukuru vijana wenzangu wa kitanzania na hata dunia nzima kwa kuyajali na kuyapa umuhimu mazingira kwani inapendeza kumwona kijana akiyapenda mazingira na tukifanya hivyo tutakuwa tumepiga hatua katika ulimwengu wa kisasa.Jukumu la kuenzi mazingira na kuyatunza pamoja na kutoa elimu ya mazingira si la serikali au taasisi peke yake bali ni la watanzania wote wenye kupenda kuona nchi ikiwa kwenye sifa nzuri.Nipo tayari kushirikia na naserikali pamoja na taasisi zote hapa nchini na nje kutoa elimu ya mazingira na kuhakikisha nchi yangu imepata sifa ndani na nje kwa kutoa elimu ya mazingira pamoja na umuhimu wake na madhara yatokanayo na uharibifu wa mazingira nitahakikisha vijana,wazee na watoto wamepata elimu hii na kupata ushindi wa mabadiliko.nitatumia uwezo wangu wote pamoja na kipaji alicho nipa mungu na ujasiri wa kuongea na kila mtu bila chuki bila uwoga na upendo uliojaa hekima.Ningeliomba bunge letu tukufu liweze kumshauri raisi ili aweze kutupatia wizara pekee inayosimama kama wizara ya mazingira inayohakikisha mazingira yana heshimiwa na kupewa umuhimu ili yaweze kustawi na kutoa taswira nzuri pamoja na kutoa ushirikiano kwa vijana wanaotoa elimu kwa kuwawezesha ili waweze kuwa na moyo wa kuhamasisha wananchi pia serikali ijitahidi kuwapa vipaumbele wana harakati wote wanaopambana na umuhimu wa mazingira kwa kuwajengea vikundi kama wajasilia mali ili waweze kulitumikia taifa kwa kutoa elimu ya mazingira kwani serikali ina vyotoa ushirikiano  ndivyo hata sisi wanaharakati tunapokuwa na moyo wa kuendelea kuhamasisha watanzania mwisho mimi kama Denis kuna kauli moja inayosema
“Yatunze mazingira nayo yakutunze” “Yatunze mazingira nayo yakutunze” “Yatunze mazingira nayo yakutunze”  Ni mimi kijana mzalendo wa chuo cha biashara Dar es salaam
Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Afrika.
DENIS HENDRY MALAMSHA
Namba za simu 0712 550 508
                             0765 002 472

2 comments:

crispaseve said...

bwana denis vipi kwenu mazingira umetunza au tu kwenye internret ndio yapooooo.acha utani makaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Anonymous said...

Insha yako ilikuwa nzuri

Powered by Blogger.