KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AMNUSURU MBUNGE WA IGALULA MFUTAKAMBA BAADA YA WANANCHI WAKE KUMJIA JUU
Wakazi
wa Kata ya Kizengi wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdulrahman Kinana alipokuwa akizungumza nao,mara baada ya kuweka jiwe
la msingi na kuzindua Ofisi ya chama hicho.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kata ya
Kizengi,Wilayani Uyui mkoani Tabora,wakati wa ziara yake iliyoendelea
mkoani humo.Kinana amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza
kero mbalimbali za Wananchi ili kuchukua hatua na kuzishughulikia,aidha
katika ziara hiyo Kinana pia ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa
na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.
Ndugu
Kinana amehutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano hadhara uliofanyika
katika Kata ya Loya,ambapo kuliibuka sintofahamu ya baadhi ya mambo
ikiwemo Mbunge wa Jimbo Igalula, Mhandisi Athuman Mfutakamba kutokuwa
na tabia ya kuwatembelea wananchi wake na kujua matatizo waliyonayo,
hali iliyosababisha Wananchi wamzomee alipopanda jukwaani kuhutubia na
kujibu maswali aliyoulizwa ambapo ilibidi Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana kuingilia kati na kurejesha hali ya utulivu na kumtaka Mbunge wa
jimbo hilo Mh,Athumani Mfutakamba kuwa na tabia ya kuwatembelea wananchi
wake.
Aidha
kauli hiyo imekuja,kufuatia Wananchi kulalamika wazi kwa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana na kutokubali utendaji kazi wa Mbunge huyo.Wananchi
hao waliweka wazi kuwa Mbunge huyo amekuwa akipiga porojo tu kwa mambo
mengi ,badala ya kuwasikiliza na kutatua matatizo yanayowakabili amekuwa
akiingia mitini.
Wananchi
hao wakatolea mfano wa Zahanati ya Kata hiyo ambayo haina jokofu la
kuhifadhia chanjo za watoto na Dawa,kwamba aliahidi kulishughulikia
lakini hakuna utekelezaji uliofanyika hadi sasa,kama vile haitoshi
Wananchi hao wakoangeza kuwa mara baada ya kuchaguliwa Mbunge huyo
aliwaahidi kuwaletea mnara wa mawasiliano ya simu za mikononi kwa muda
wa siku 100,ambalo ndio tatizo kubwa kwa kata hiyo ya Loya,lakini
hakulitekeleza mpaka sasa.
Hata
hivyo katika kuweka mambo sawa kwa Mbunge huyo,katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
kinana aliwaeleza wananchi kuwa atawasaidia kufuatilia suala hilo la
mawasiliano,na pia amewaahidi kuwanunulia jokofu hilo kwa wananchi wa
Kata ya Loya wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye,akiwahutubia wakazi wa Kata ya Kizengi waliojitokeza kwa wingi,Wilayani Uyui mkoani Tabora,kwenye mkutano wa hadhara.
Mbunge
wa Jimbo la Igalula,Mh.Athuman Mfutakamba,akieleza maendeleo ya miradi
mbalimbali iliyotekelezwa na chama cha CCM,kufuata Ilani ya chama
hicho,katika Lijiji cha Loya,Wilayani Uyui mkoni Tabora.
Mwenyekiti
wa CCM,Wilaya ya Uyui,Mussa Ntimizi akizungumza na Wananchi wa Kata ya
Kizengi wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa ajili
ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya chama hicho na kuzungumza na
wananchi.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Loya,Wilaya ya Uyui.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani) akisomewa taarifa fupi mara
baada ya kukagua ujenzi wa nyumba mbili za waalimu wa Shule ya Sekondari
Lutende,Wilayani Uyui mkoani Tabora.
Ndugu
Kinana akizungumza na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Miyenze,ambapo
paalibulika na hoja ya mgogolo mkubwa wa wafugaji na Wahifadhi uliodumu
kwa muda mrefu.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi kenyew Ofisi ya CCM,kata ya Loya wilayani Uyui mkoani Tabora.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya
ya Uyui,Mussa Ntimizi na Mbunge wa Jimbo la Igalula,Athumani Mfutakamba,
wakisalimiana na baadhi ya vijana wa michezo mara walipowasili katika
kata ya Loya,kwa ajili ya mkutano wa hadhara na wananchi.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Loya,katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo,Wilayani Uyui
mkoni Tabora.
Katibu wa NEC,Itikadi Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akihutubia Wananchi,katika kijiji cha Loya,Wilayani Uyui mkoni Tabora.
Vijana
wa Sungusungu wakicheza wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana alipokuwa akiwasili katika kata ya Kizengi,wilayani Uyui kuweka
na kuzindua Ofisi ya chama hicho na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Vijana
wa Sungusungu na Baadhi ya Wazee wa Kata ya Kizengi wakimpokea Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake walipokuwa wakiwasili katika
kata ya Kizengi,wilayani Uyui kuweka na kuzindua Ofisi ya chama hicho na
kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment