Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji Makaa ya Mawe,
Tancoal, Graeme Robertson, wakati alipotembelea mradi
wa Uchimbaji Makaa ya Mawe unaoendelea eneo la Ruanda
Wilaya ya Mbinga, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Ruvuma jana.
Ukifanywa utafiti wa
kugundua upatikanaji wa makaa ya mawe kabla ya kuanza uchimbaji.
Makaa yakichekechwa na
kupatikana makaa bora na mabaki kuwekwa mahala maalum palipoandaliwa ili
kuepuka uchafuzi wa mazingira.
Magari
yakiwa mgdini chini yakiendelea na kazi ya uchimbaji wa Makaa ya mawe
hayo ambayo soko lake kubwa limekuwa ni nje ya nchi kama Zambia, Ghana
na kwingineko.
Mke
wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal (katikati) akiwa na Mke wa Mkuu wa
Mkoa wa Ruvuma (kushoto) na Mke wa Mbunge wa Mbinga, wakati
walipotembelea shughuli hiyo ya uchimbaji.
Sufianimafoto, naye hakusita
kupiga picha ya kumbukumbu mahala hapa muhimu kwenye utajiri mkubwa wa
Taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment