LAKI MBILI WAJITOKEZA MPANGO WA "WEZESHWA NA SAFARI LAGER"





SAFARI LAGER YATANGAZA
KUSALIA MAJUMA MATATU YA MPANGO WA KUWAWEZESHA
WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO NCHINI. “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”
Dar es Salaam,Alhamisi
February16, 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari
Lager leo imetangaza maendeleo ya kampeni ya aina yake ya kuwatafuta na
kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo katika shindano la wezeshwa na
Safari Lager na unaweza kupata ruzuku ya kusaidia kuona
njiaya mafanikio katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Arusha ambapo sasa
zimesalia siku 21 kabla ya zoezi hilo kufungwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dasr
es salaam,Menejawabiaya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema Bia ya
safari Lager ilizindua program maalum ya kuwawezesha ya
kufanikisha kuwawezesha wajasiriamali wadogowadogo nchini kupitia
programu ya wezeshwa na Safari lager Novemba 24 jijini Dar Es Salaa
ikiwa na lengo kuu la kuwasaidia wamiliki wa biashara ndogondogo naza
kati kukuza biasharazao,
Alisema
programu hiyo ilizinduliwa katika kanda kuu nne za Tbl ambazo ni kanda
ya Dar Es Salaa,Kanda ya Ziwa,kanda Kaskazini na kanda ya nyanda za juu
kusini ambapo wamiliki wa biashara ndogondogo walipaswa kuchukua fomu
maalum toka katika bohari na viwanda vya Tbl katika mikoa yao au pia
kuchukua fomu kwenye tovuti www.wezeshwa.co.tz au kutuma barua pepe kwenda info@wezeshwa.co.tz au
unaweza kupiga simu nambari 0763 600041 (Dar es Salaam) 0763600042 (Arusha) 0763
600044 Mwanza) na 0763 600045 (Mbeya) namwishowakurudishafomuni 02Machi
2011
Alisema kwa hivi sasa
programu hiyo inaelekea ukingoni ambapo hivi karibuni jopo la majaji
walibobea katika elimu ya uendeshaji wa biashara wataanza mchakato wa
kupitia fomu zote zilizotumwa ili kuweza kupata washindi kwa kila
kanda.
Leo hii tunapenda
kuwafahamisha watanzania kuwa zimebaki takribani majuma matatu kabla ya
pazia la kuchukua na kuresha fomu kufungwa rasmi tarehe 02.03/2012 saa
sita usiku hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wale
wamiliki wa biashara ndondogo waliochukua fomu kurejesha katika vituo
husika mapema na pia kwa wale ambao bado hawajachukua maamuzi ya
kushiriki kufanya maamuzi hivi sasa maana muda umebakia mchache sana na
kama tunavyofahamu sote Safari Lager imeandaa kiasi cha Shilingi
milioni mia mbili ( 200,000,000) ambazo zitatolewa kwa wamiliki wa
biashara kama ruzuku na pia wataalamu wetu watafanya mchakato wa
kuwawezesha hao washindi ishirini kwa kila kanda kuweza kuwapatia
semina na elimu ya ujasiriamali na namna ya kuendeleza na kukuza
biashara zao,Alisema bwana Shelukindo.
No comments:
Post a Comment