


Rais Jakaya Mrisho
Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua matofali ya kisasa
kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa vijana 380
toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha vijijini,
Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.
Kambi
hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa
mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29,
itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha
Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya
mbogamboga wilayani Rufiji.

Rais
Kikwete
ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi hizo na kutaka mikoa mingine
iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa kuweza kujiajiri wenyewe.
Ameahidi
kuendelea kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja
kama hazina nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la
ajira.
Rais
Kikwete
ametoa mashine za kufyatulia matofali ya kisasa 76 ambapo kila moja
kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa mashine mbili mpya na
waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu. Pia Amewapa vijana
hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100), viatu vigumu (gum
boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake.
No comments:
Post a Comment