DR CONRAD MURRAY AKUTWA NA HATIA KIFO CHA MICHAEL JACKSON

Aliyekuwa Daktari wa Michael Jackson, Dr Conrad Murray amekutwa na hatia ya kutoa dose ya dawa kali za usingizi zilizopelekea kifo cha nguli huyo wa Pop. Dr Murray 58 amepatikana na hatia hiyo na hivyo anasubiri hukumu rasmi mnamo Nov 29 mwaka huu.
kwa kosa alilofanya dokta huyo ambaye Michael alikuwa akimlipa milioni 170 kwa mwezi,anategemewa kupelekwa jela kwa miaka minne huku akipoteza leseni yake ya utabibu. Mahakama imekataa kumpatia dhamana na hivyo Dr Conrad amerudishwa rumande akisubiri kujua rasmi gereza atakalokwenda kutumikia kifungo chake cha miaka 4 ifikapo tareh 29 Novemba 2011.
No comments:
Post a Comment