UGANDA YADHAMIRIA KUPITISHA SHEHENA ZA MIZIGO KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI
wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege amesema, nchi
hiyo imedhamiria kupitisha shehena nyingi za mizigo yao katika bandari
ya Dar es Salaam kwa sababu ya vivutio vingi vilivyopo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kufanya ziara katika bandari ya
Dar es Salaam Mhandisi Mtege amesema bandari hiyo ni njia rahisi kwao
ya kupitisha mizigo yao na pia usafiri wa kutumia njia ya maji ni wa bei
nafuu.Alisema
vivutio vilivyopo katika bandari ya Dar es Salaam hawaoni sababu
itakayo wakwamisha kupitisha mizigo yao na kuendeleza uchumi wa nchi
yao.
"
Kufika Bandari ya Dar es Salaam ni mara yangu ya kwanza lakini
nimeshuhudia mambo mengi ikiwamo maboresho ya miundombinu hivyo
napongeza Serikali ya Tanzania ambazo zimechukuliwa hasa za kufungua
njia ya ukanda wa kati jambo lililorahisisha kufika kwa mizigo kutoka
Dar es Salaam kwenda Uganda," alisema Monica.
Amesema tayari wamejiandaa kuhakikisha wanasafirisha shehena kwa wingi kutoka Uganda kuja Dar es Salaam.Amesema tayari wameandaa makampuni makubwa yenye nia ya kuja Dar es Salaam kupitia njia ya ukanda wa kati.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Lydia Malya amesema, tayari
bandari wameanzisha kikosi kazi maalum ili kuhakikisha wanapata mizigo
mingi zaidi ya Uganda.Amesema watatumia fursa mbalimbali kutangaza njia hiyo kwa faida ya nchi mbili.
Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege akizungumza
katika mkutano wa menejimenti ya TPA wakati alipotembelea bandari hiyo
jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na
Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akitoa maelezo wakati Waziri wa
Uganda alipotembelea banadari ya Dar es Salaam
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Banadari , Mhandisi Karim
Mataka akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa ujenzi na Uchukuzi wa
Uganda alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignatus
Rubaratuka akizungumza kuhusiana na mamlaka hiyo kuhakikisha inatoa
huduma bora kutokana na ushirikiano kati ya Uganda na Tanzania
No comments:
Post a Comment