NITAREJESHA DIRA YA MPIRA WA MIGUU KUWEZESHA SERIKALI KUPATA MAENDELEO KATIKA SEKTA YA MICHEZO- ALLY MAYAY
Na Karama Kenyunko Globu ya jamii.
Mgombea
urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ali Mayay amesema kuwa
katika uongozi wake atahakikisha dira ya mpira wa miguu inarejea katika
mstari na kuiwezesha nchi kupata maendeleo makubwa katika sekta hiyo.
Mayay
amesema hayo leo alipokuwa ananadi sera zake katika siku ya kwanza ya
uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti
12, mkoani Dodoma. Amesema kuwa kwa sasa hakuna dira ya mpira wa miguu
na ndio chanzo cha kuwa na maendeleo duni ya mpira kulinganisha na nchi
zingine ambayo kwa sasa zinafaidi matunda baada ya kuanzisha na
kutekeleza dira hiyo.
“Kwa
sasa wachezaji wengi wa Zambia wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi,
timu yao Taifa inafanya vizuri, Tanzania ina wachezaji wengi wenye
vipaji, lakini hakuna dira na kusababisha wao pia kukosa dira katika
fani yao,” alisema Mayay.
Alisema
kuwa akiwa kama mchezaji, ameweza kuona changamoto mbalimbali za mpira
wa miguu na kuamua kugombea nafasi iliyo ili kuzitatua na lengo lingine
ni kujenga taasisi imara kwa kutumia rasilimali zilizopo kwani tatizo
si vipaji, bali ni aina gani ya uongozi unaosimamia mpira wa miguu.
Wachezaji
mbalimbali waliong’aa katika medani ya soka hapa nchini, wamepigia
chapuo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Ali Mayay
kuchaguliwa katika nafasi ya urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
Mgombea
huyo ambaye ni chaguo la wachezaji wa zamani nchini aliungwa mkono na
mshambuliaji nyota wa zamani wa Klabu ya Simba, Zamoyoni Mogella ambaye
alisema TFF inahitaji mtu kama Mayay anayejua matatizo ya mpira wa
miguu kwani ameucheza huo mpira.
Mogella
ambaye enzi zake alipewa jina la “Golden Boy” na “Morgan” alisema kuwa
wanahitaji kuurudisha mpira kwa wenyewe huku wakiwaomba wagombea
kumchagua Mayay kwani ni wakati wa mabadiliko kwa wadau wa soka nchini
kwa kumchagua Mayay ambaye anavigezo vyote katika masuala mbalimbali ya
soka na uongozi.
“Mayay
ni dira ya soka Tanzania, amecheza soka kuanzia shuleni, katika hatua
ya vilabu mpaka timu ya Taifa, anajua nini cha kufanya ili kuleta
maendeleo ya soka nchini,” alisema Mogella.
Mchezaji
wa zamani wa Yanga Mohamed “Adolph” Rishad naye alisema kuwa Mayay ni
suluhisho sahihi kwa maendeleo ya soka nchini na si wagombea wengine
zaidi wachezaji wa mpira wa miguu wametengwa katika soka na kukosa
mwamko katika mchezo ambao wanaupenda.
Amesema
kuwa kwa sasa Tanzania ina matokeo mabaya katika soka la kimataifa ni
kukosa uongozi wenye mapenzi ya mchezo pamoja na Tanzania kuwa na vipaji
vingi vya soka.
No comments:
Post a Comment