Header Ads

DAWASCO WAZINDUA HUDUMA YA MAJI MTANDAONI


Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limezindua mfumo mpya wa Mawasiliano ambao unalenga kumrahisisha mteja kupata na kutoa taharifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu amesema lengo la mfumo huu ni kumuweka mteja karibu kihuduma.

"Smartphone itamuwezesha kila mwananchi kupakua huduma hii hili aweze kupata huduma kwa kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO Ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajiri mteja atatumiwa neno la Siri" amesema Kingu.

Naye, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi. 
 
“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.

Amesema kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akionyesha mfumo wa Huduma Mtandaoni unavyofanya kupitia simu za mkononi
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akifafanua jambo kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa mawasiliano katika simu za mikononi inayowawezesha kupata taarifa zote muhimu za shirika hil kwenye simu. Pamoja naye ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro.
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kuzindua huduma ya simu mtandaoni

Waandishiwa habari waliohudhuria mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.