MAREKANI KUPITIA SHIRIKA LAKE LA MISAADA LA USAID YAIPATIA TANZANIA DOLA MILIONI 225 KWA AJILI YA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO
Siku
moja baada ya Marekani kutangaza kutoa fedha za nyongeza katika mwaka
ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini,
nchi hiyo imetiliana saini na Wizara ya Fedha na Mipango makubaliano ya
kutoa Dola Milioni 225.
Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na Utawala bora.
Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini Bw. Andy Karas.
Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Bw. Doto James ameishukuru Marekani kwa kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na Tanzania na amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi.
Nae Bw. Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani wanafurahishwa na kuendelea kwa ushirikiano mwema kati yao na Serikali ya Tanzania katika maendeleo na ameahidi kuwa ushirikiano huo utadumishwa.
Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza
kushoto)akisaini mkataba wa Makubaliano (Strategic Assistance Agreement
)na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy
Karas(katikati) kuhusu utoaji wa fedha hizo dola za kimarekani Millioni
225 , tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
Wakwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi
Patterson akishuhudia.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto)
akibadilishana mkataba ya makubaliano (Strategic Assistance Agreement)
na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas
katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto)
akipiga makofi pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani
nchini USAID Andy Karas(katikati), na Kaimu Balozi wa Marekani hapa
nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano
(Strategic Assistance Agreement ) katika ofisi za Hazina jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Kaimu Balozi
wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini
mkataba huo utakaowezesha Tanzania kupatiwa fedha hizo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Mkurugenzi wa
Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas mara baada ya
tukio hilo la mkataba wa makubaliano katika Ofisi za Hazina jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment