JAFO: ZOEZI LA HOSPITALI TEMBEZI LIFANYIKE MIKOA YOTE
NAIBU
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Makatibu
tawala wa mikoa yote Tanzania bara kuratibu zoezi la Hospitali tembezi
katika mikoa yao ili kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kupata huduma
ya kibingwa.
Jafo
ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizindua huduma za hospitali tembezi
kwa wilaya ya Chemba na Kondoa zoezi ambalo limefanyikia mjini Kondoa.Mpaka
sasa zoezi hilo limeshafanyika katika wilaya ya Kongwa, Mpwapwa,
Chamwino na sasa linaendelea kwa wilaya za Chemba na Kondoa.
Akizindua
huduma hiyo, Jafo ameumwagia sifa uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa
kuratibu vyema zoezi hilo ambapo zaidi ya wagonjwa 8,000 wamefanyiwa
uchunguzi huku 500 wakifanyiwa upasuaji mdogo na mkubwa.
Amewataka
wananchi wa wilaya hizo kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za
kibingwa huku akiwataka kupima tezi dume kwa kuwa umekuwa ugonjwa tishio
kwa wanaume.
Ameeleza kuwa huduma hizo za kibingwa zinatolewa kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha wananchi wasio na uwezo kupata matibabu.Jafo amewapongeza madaktari bingwa wa mkoa wa Dodoma kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewataka wengine waige mfano wa Dodoma.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi
wa Hospitali tembezi katika wilaya ya Kondoa na Chemba.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Dk.James Kiologwe na viongozi wa wilaya ya Chemba na
Kondoa.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya za Kondoa na Chemba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
Wananchi waliofika katika uzinduzi wa hospitali tembezi.
No comments:
Post a Comment