DKT. ALOYCE NZUKI AFUNGUA WARSHA YA KUKUSANYA MAONI YA WADAU WA KANDA YA KATI KWA AJILI YA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA UTALII YA MWAKA 1999 MJINI DODOMA
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki
akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya kukusanya maoni
ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya
Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini
Dodoma leo.
Dkt.
Nzuki amesema ipo haja sasa kwa Sekta za Umma kuona umuhimu wa kuwekeza
moja kwa moja katika biashara ya utalii nchini hususani katika huduma
za malazi na usafiri ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ya moja kwa
moja na kuongeza zaidi kwenye pato la taifa.
Alisema
kwa kuimarisha usafiri wa anga kutawezesha usafiri wa watalii moja kwa
moja kutoka kwenye soko na kuwaleta nchini huku wakilipia gharama zote
hapa nchini tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya makampuni ya nje
hulipwa fedha kiasi nje ya nchi na hivyo kuikosesha Serikali mapato
kupitia ushuru unaotozwa na TRA.
Alisema
sio lazima Serikali iwe inasimamia moja kwa moja utoaji wa huduma hizo
kwa kuwa upo uwezekano wa kutumia makampuni makubwa hata ya nje ya nchi
kuja kuendesha huduma hizo kwa ufanisi zaidi hapa nchini.
Naibu
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia)
na wadau wengine wa sekta ya utalii wakimsikiliza Prof. Raphael Mwalyosi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia) wakati akiwasilisha mada kuhusu
Hoja ya Marekebisho ya Sera ya Utalii ya Mwaka 1999 katika warsha ya
kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kupitia upya Sera hiyo
iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na
Shirikisho la Utalii mjini Dodoma leo.
Kamu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Deograsias Mdamu akizungumza katika warsha ya siku moja ya kukusanya
maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii
Tanzania mjini Dodoma leo.
Picha
ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.
Aloyce Nzuki (katikati waliokaa) na wadau wa sekta ya utalii katika
warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa
ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999
iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki
ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.
Baadhi
ya wadau wa sekta ya utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha ya
kukusanya maoni ya wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya kupitia upya Sera ya
Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na
Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii
Tanzania mjini Dodoma leo.
Baadhi
ya wawezeshaji wa hafla hiyo ambao ni Maafisa Utalii kutoka Wizara ya
Maliasili na Utalii wakisikiliza moja ya mada katika warsha hiyo.
Baadhi
ya wadau wa warsha hiyo wakisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mgeni Rasmi
ambaye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce
Nzuki.
Baadhi ya wadau wa warsha hiyo.
Baadhi
ya Washiriki wa warsha hiyo kutoka Mikoa ya Kanda ya Kati iliyofanyika
mjini Dodoma. (NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
HOTUBA YA UFUNGUZI YA NAIBU KATIBU MKUU, WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, DKT. ALOYCE NZUKI
HOTUBA YA KAIMU MKURUGENZI IDARA YA UTALII, DEOGRASIAS MDAMU
No comments:
Post a Comment