ZAIDI YA SH BILIONI 200 KUWANUFAISHA VIJANA NCHINI
Filbert Rweyemamu,Arusha
Benki
ya Dunia imetoa Sh 200 Milioni ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi
kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo
viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara
baada ya kuhitimu elimu.
Akizungumza
katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia
kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za
kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.
Alisema
kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika
masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili
iliyochini ya taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo
vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine(Sua).
Mkurugenzi
wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia,
Bella Birds alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza
ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia
uchumi wa viwanda.
Bella
alisema inakadiriwa kuwa vijana milioni 1 huitimu katika vyuo na kuingia
katika soko la ajira kila mwaka hivyo anatarajia kuwa nafasi za ajira
kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo zitashirikiana
vyema na serikali .
Makamu
wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Karoli Njau
alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa
malengo yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa
ujuzi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye
amesema kuwa kulikua na upungufu mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini
kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo kulazimu waajiri kuajiri
watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo mradi huo
utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la
ajira.
Waziri
wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili
kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya
umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi
wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa
na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho
Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa David Mwakyusa
na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .
Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho
Waziri
wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua mradi wa
Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu
kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi
,Burundi na Somalia Bella Bird.
No comments:
Post a Comment