ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KUANZA KESHO
WADADISI
wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18 wameaswa kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la
kuorozesha kaya linalotarajia kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi
ya utafiti huo.
Akizungumza
wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa
wadadisi hao, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji
wa kaya, ni lazima wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na
kufuata taratibu zote za Utumishi wa Umma.
“Ofisi
ya Taifa ya Takwimu inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa ajili ya
kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Natumaini mtatii na kuheshimu
maadili ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha kazi hii kwa
ufanisi,” amesema Slyvia Meku.
Amesema
Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya litafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara
kwa takribani siku 15 kuanzia kesho Julai 11, 2017 na baadae kufuatiwa
na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza mwezi Desemba, 2017.
Sylvia
Meku amesema utafiti huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa
kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa
Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha umasikini nchini.
Meneja
wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku akizungumza wakati wa
mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili
ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania
Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa
muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
Baadhi ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Takwimu za Jamii
na Watu Bi. Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa mafunzo ya Wadadisi
watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku
kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
Baadhi
ya Wadadisi wakiwa kwenye gari wakielekea Kata ya Mchikichini, Ilala na
Kawe jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa
vitendo kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya
litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11
Julai, 2017.
Baadhi
ya Wadadisi wakielekezwa namna ya kutumia ramani wakati wa kufanya
mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo na Mtalaam wa Ramani Jumanne
Msuya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) kwa ajili ya maandalizi ya
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku
kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA)
No comments:
Post a Comment