WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TANO
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi
Mzee Mtopa wakati alipowasili Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi, katika
ziara ya kikazi ya siku tano,(katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfey
Zambi, Julai 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewasili Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku
nne, akiwa mkoani humo Waziri Mkuu ameanza ziara yake katika wilaya ya
Liwale kwa ajili ya kukagua shughuli za maendele na jioni ya leo atukuwa
na mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa Liwale pamoja na
kusikiliza kero zao
Waziri
Mkuu ameongozana na Mke wake Mery Majaliwa ambapo walipokelewa na Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi pamoja viongozi wa wilaya za Mkoa wa
Lindi ambao walifika katika mapokezi katika uwanja wa ndege wa
Nachingwea.Waziri Mkuu hapo kesho anatarajia kuendelea na ziara yake wilayani Ruangwa.
No comments:
Post a Comment