Msanii
wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego akifanya yake kwenye Shoo ya Wapo
iliyofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Zakhem jijini
Dar....Akiimba sambamba na mashabiki zake
Msanii Kala Jeremiah alivyowarusha mashabiki kwenye Shoo ya Wapo.Msanii Kala Jeremiah alivyowarusha mashabiki kwenye Shoo ya Wapo.
Mashabiki wakiwa na furaha ya burudani.
Msanii Barnaba na Shilole wakifanya yao kwenye jukwaa la Dar Live jana usiku.
Msanii Shilole akikata nyonga na shabiki wake.
Mchekeshaji Mkali Wao na Ninyetwa Ebitoke wakionesha uwezo wao.
DJ Zero akitoa saluti kwa mashabiki wake.
ONESHO kabambe la Wapo Concert lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani
ya ukumbi wa burudani wa Taifa wa Dar Live hakika liliacha historia kwa
mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia onesho hilo ambalo ni la aina
yake kufanyika ndani ya ukumbi huo.
Onesho
hilo lililowashirikisha wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya, Nay
wa Mitego, Barnaba, Shilole ‘Shishi Bay’, Kala Jeremiah na mabingwa wa
vichekesho hapa nchini, Mkali Wenu na wenzake, hakika lilikuwa la aina
yake na liliacha simulizi kubwa kwa mashabiki waliojitokeza
kulishuhudia.
Onesho hilo lililoongozwa na DJ Ziro na DJ Max wa Dar Live ambao
walizikonga nyoyo za mashabiki, lilianza kwa shamrashamra kwa wasanii
waliopanda jukwaani kupiga shoo za utangulizi.
Nusura
baadhi ya mashabiki hao wavunjike mbavu kwa vicheko kufuatia vichekesho
vilivyoletwa na Mkali Wenu na wenzake kwani jamaa hao ni noma kwa
kuvunja mbavu watu, hata walipomaliza kutoa burudani mashabiki waliwaita
warudie tena nao wakafanya hivyo.
Ilikuwa kama mvua inataka kutibua onesho hilo lakini mashabiki
hawakujali mvua ambayo ilikuwa inanyesha kwani waliendelea kula shangwe
bila kujali mvua iliyokuwa inamwagika kwa wingi.
Hata
Barnaba alipopanda jukwaani na wimbo wake wa Milele, aliwakuta
mashabiki hao wameshapagawa na yeye kuwaongezea mzuka kwa burudani ya
nguvu.
Mashabiki hao walizidi kupagawa zaidi baada ya Barnaba kumpandisha
jukwaani Shishi Baby na kuimba nae pamoja wimbo mpya wa Shilole wa
Hatutoi Kiki.
Shishi Baby alimpisha Kala Jeremiah ambaye aliwakuta mashabiki hao
wamewehuka kwa burudani, naye akaongeza ngoma juu ya ngoma.
Ukumbi
ulirindima zaidi baada ya Nay wa Mitego kuvamia jukwaa kwa wimbo wake
wa Muziki Gani, mashabiki wakavamia jukwaa huku baadhi wakitaka japo
wamguse.
Nay aliweka historia kubwa ndani ya ukumbi huo wa taifa wa burudani
uliopo Mbagala jijini hapa alipowatendea haki mashabiki hao kwa
kuwadondoshea ngoma zake zote mwanzo mwisho.
(PICHA/HABARI: ISSA MNALY/GPL)
Wapo Concert: Nay wa Mitego, Shilole, Waandika Historia Dar Live
Reviewed by
bamiza
on
9:47 AM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment