BALOZI SYLEVESTER MABUMBA, BALOZI WA TANZANIA VISIWANI KOMORO AWASILISHA NAKALA YA HATI ZAKE ZA UWAKILISHI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOMORO, MHE, MOHAMED BACCAR DOSSAR
Mhe.
Sylvester Mabumba Balaozi wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa
Visiwa vya Komoro jana tarehe 09 Mei aliwasilisha nakala za hati zake za
uwakilishi kwa Mhe. Mohambed Baccar Dossar, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Komoro. Hafla hiyo ilifanyika siku hiyo hiyo ambayo Mhe. Balozi
aliwasili Visiwani Komoro jambo ambalo linaonesha jinsi gani nchi hizi
mbili zimedhamiria katika kuboresha na kukuza mahusiano yaliopo baina
yao.
Katika hafla hiyo Mhe. Dossar alichukua fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Balozi Mabumba Visiwani Komoro na kumtakia kila la kheri katika kipindi chake ambacho atakuwa Balozi Visiwani hapa. Aidha Mhe. Waziri alimuahidi Mhe. Balozi Mabumba kuwa nchi yake itampatia ushirikiano maradufu na kwamba milango yake ipo wazi muda wowote ambapo Mhe. Balozi atakuwa na shida ya kuonana nae na kufanya mazungumzo.

Kwa
upande wake Mhe. Balozi Mabumba alionyesha furaha yake kwa kumuelezea
Mhe. Waziri kuwa amejiskia faraja sana kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa
Pili kuiwakilisha Tanzania Visiwani Komoro na kwamba anaimani kuwa
Serikali ya Komoro itampatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza
majukumu yake.
Aidha
Mhe. Balozi Mabumba alieleza kuwa uhusiano uliopo baina ya Tanzania na
Komoro ni wa Kihistoria na unapaswa kudumishwa. Mhe Balozi alimueleza
Mhe. Waziri kuwa moja ya agenda zake za mwanzo ambazo anataka kutekeleza
ni ile ya utiaji saini wa Mkataba wa Kudumu wa Ushirikiano baina ya
Tanzania na Comoro (Joint Permanent Commission).
No comments:
Post a Comment