TUJIKUMBUSHE KUHUSU MAREHEMU FAZA NELLY: MSANII WA HIPHOP TANZANIA
Jumatatu ya 29 March Mwaka 2006
Fans wa Swahili Hip hop World wide dunia nzima walikua na simanzi
kutokana na Taarifa za kifo cha Nelson Chrizostom Rutta/maarufu kama
Faza Nelly ambae alikufa kutokana na Majeraha ya kuchomwa na Kisu mara
tisa na Jirani yake akijulikana na kama Moses Yohana Kilevo,
Baadhi
ya watu watakua wanajiuliza Faza Nelly ni nani? Kuna majibu mengi
katika swali hilo, lakini Jibu Katika Music Industry ni kwamba Faza
Nelly ni Mwanzilishi wa kundi la XPlastaz, Kundi la Rap kutoka A-town
ambalo lilikua na Memberz sita wengi wao wakiwa ni ndugu, kundi
lilijilikana world wide kupitia Concert tours walizofanya Brazil,
Holland, U.K na sehem nyingine duniani without forgetting their Mama
land Tanzania, na umaarufu wa X-Plastaz unatokana na kwamba walikua
wakitumia Hardcore Beats, Swahili Rhymes na Traditional Maasai Music
ambayo huimbwa na Maasai Warrior akiitwa Merege, Memberz wa X-plastaz ni
Ziggy Lah, G Ssan,Steve, MeregeDiney na The late Faza Nelly,
Kifo cha Faza Nelly
Kama
nilivyosema mwanzo mchizi aliyehusika na Mauaji ya Faza Nelly alikua ni
jirani yake moses yohana Kilevo, Jirani huyo alikua na Historia ya
kuwatishia jirani zake siku zote kama vile kuandika kwenye Kuta za
kitaani kwao kuwa yeye ni muuaji/ Iam a Killer bila kujali hata watoto
wake wanaona maandishi hayo na inaweza kuwaathiri watoto hao…
Mambo
kama hayo ya kutokueleweka kwa Jirani huyo yaani Moses Yoahana Kilevo
yalisababisha majirani wote kuungana na Kusgn barua ya kuomba kwa
serikali ya mtaa kum’hamisha kitaani hapo kwa kilicho elezwa kuwa hawana
imani nae kutokana na vitisho vya kuua alivyokua anavitoa kwa wenzake
mara kwa mara,,,,,
Kuna
siku moja, mmoja kati ya rafiki wa Faza Nelly ambae alikua akiishi
nyumba moja na Faza Nelly na Moses Pia, anaitwa Musa alijaribu kuongea
na muuaji lakini baadae akaja kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za uongo za
kumkaba na Kumwibia Moses, kitu ambacho hakikuwa kweli, Faza Nelly
akajaribu kumtetea Musa polisi kuwa si mwizi, na kuelezea ukweli juu ya
uzushi ule na kwamba hata
Majirani wote wanalijua hilo, ndipo polisi wakamwambia basi aende na
Majirani kutoa ushahidi, Faza Nelly akarudi home na kujaribu kuzungumza
na Muuaji Moses ambae alikasirishwa na Tukio hilo na kutaka kupigana na
Faza Nelly, ili kuepusha ugomvi Nelly aliamua kurudi chumbani kwake,
kulala, sekunde chache baadae Muuaji Moses akamjia na Kisu kisu kikubwa
na Kumchoma nacho Faza nelly Sehemu tofauti za mwili wake mara Tisa,
ikiwemo puani, begani na Kwenye Mapafu.
Kwa
mujibu wa familia yake na Mazingira, inasemekana hakukua na Mapigano
kabisa katika Tukio hilo, Na Faza Nelly alikua ni Mtu amani/ mpole,
Mkarimu ambae hakuweza kumdhuru mtu yeyote, na hii ilijidhihirisha
kwenye Lyrics zake kama katika Tittle ya ngoma yake inaitwa NINI DHAMBI KWA MWENYE DHIKI, na ndio maana hata aliposhambuliwa na Muuaji Moses Kilevo alishindwa kujitetea, ukizingatia pia alishambuliwa kutoka mgongoni,
Baada
ya Tukio hilo Nelly akaspend siku mbili Hospitalini akiwa anatumia
mashine za kupumulia, madaktari walijaribu kuokoa maisha yake lakini
walipotaka kumfanyia Surgery kwa mara ya pili, ghafla hali yake ikawa
mbaya sana na kufariki mbele ya madaktari na Rafiki yake Musa.
Muuaji…Moses Yohana Kilevo
Alikua
ni baba wa familia ya watoto wawili na mke mmoja, alikua ni mtu timamu
yaani hakua kichaa, na alijulikana kwa vitendo vyake vya vitisho kwa
majirani zake, hakua mstaarabu kabisa, baada ya tukio hilo la kikatili
Muuaji huyu alikimbia na hajaonekana mpaka leo, Polisi bado wanafanya
upelelezi na kuna uwezekano mkubwa kuwa alikimbilia Nairobi kwani huko
ana ndugu, kipindi kile familia ya Faza Nelly iliweka laki tano kwa mtu
yeyote atakaye fanikisha kukamatwa kwa muuaji huyo.
Mazishi
Mazishi
ya The late Faza Nelly yalifanyika siku tano baada ya kifo chake, na
kuchelewa kwa mazishi yake kwa kuwa Familia yake ilibidi kumsubiri mdogo
wake Faza Nelly, anaitwa G-San ambaye anaishi nje ya Nchini Markeani,
na soon as alpofika Arusha, hatimaye mwili wa Faza Nelly ukahifadhiwa
katika Makaburi yaliyopo Njiro Arusha, zaidi ya watu elfu moja walimzika
Mwana hip hop huyu, vijana kwa wazee, simanzi ilitawala Katika
Ulimwengu wa Hip Hop, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.
Mungu ailaze Roho ya Faza Nelly mahali pema peponi…Amen
No comments:
Post a Comment