TADB YAJIPANGA KUSHIRIKIANA NA WADAU
Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kuanzisha
mtandao mpana wa majadiliano na wadau mbalimbali, zikiwemo Wizara
zinazohusika na Kilimo na Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi,
ili kukubaliana vipaumbele na namna ya kushirikiana katika kufanikisha
utekelezaji wa majukumu ya TADB.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati akichangia mada
wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo linaloendelea katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Bw. Assenga alisema kuwa kwa kushirikiana
na wadau mbali mbali wa maendeleo kutachagiza kusaidia uwekezaji mkubwa
kwenye Sekta ya Kilimo, na kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
Alitolea
mfano wa juu ya umuhimu wa ushirikiano na wadau mbali mbali kwa kutaja
utekelezaji wa vitendo wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya
Tanzania na Morocco kwa kuingi Mkataba na Benki ya Kilimo ya Morocco
(yaani Kundi la Utoaji wa Mikopo kwenye Kilimo nchini Morocco) ambayo
yamelenga katika maeneo mbali mbali yahusuyo maendeleo ya kilimo,
hususan upatikanaji wa fedha.
Kwa upande wa mikopo, Bw. Assenga, TADB
imekuwa
ikitoa mikopo ya muda mfupi; muda wa kati; na muda mrefu kwa Wakulima
wadogo wadogo, wa kati na wakubwa,
hususan kuziba pengo la upatikanaji wa fedha kwenye minyororo ya
thamani katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu
(ufugaji nyuki).
Bw. Assenga amesema kuwa mpaka sasa Benki imekopesha jumla ya shilingi 6.5 Bilioni kwa
kukopesha vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575.
“Vile
vile Benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 336 vya wakulima
wadogowadogo vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika
mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga. Hivyo kuwezesha jumla ya vikundi 19
kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi
vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali
ya kuweza kukopesheka,” aliongeza Bw. Assenga.
Mwezeshaji wa wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo Prof. Andrew Temu (Kulia) akizungumza wakati wa Kongamano
hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kulia) na
Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT – CTF), Dkt. John Kyaruzi
(Kushoto) wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Wadau walioshiriki Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kulia)
akichangia mada wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo
katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa
Mfuko Kichocheo wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT – CTF),
Dkt. John Kyaruzi.
Katibu
Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania
(SAGCOT – CTF), Dkt. John Kyaruzi (Kulia)
akichangia mada wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo
katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Kushoto ni Bw. Alex Mkindi.
Wadau wakichangia hoja mbalimbali wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo, Prof. Andrew Temu (Aliyesimama) akizungumza na wadau waliojitokeza
wakati wa Kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment