MKURUGENZI TAASISI YA ILTC YA JIJINI MWANZA AOMBA SERIKALI KUZISAIDIA TAASISI BINAFSI ELIMU.
Na George Binagi-GB Pazzo
Taasisi
ya lugha ya International Language Traing Centre iliyopo Isamilo Jijini
Mwanza, imeiomba serikali kuzisaidia taasisi binafsi za kelimu nchini
ili kutimiza vyema wajibu wake.
Mkurugenzi
wa taasisi hiyo, Mwalimu Charles Mombeki (pichani), ameyasema hayo
wakati akizungumza na Lake Fm ya Mwanza na kuomgeza kwamba ikiwa
serikali itafanya hiyo, itazisaidia taasisi hizo kutekeleza vyema wajibu
wa kutoa elimu bora kwa wananchi.
Amesema
si vyema serikali kuzifungia taasisi binafsi za kielimu ikiwemo shule
na vyuo pindi zinapokabiriwa na changamoto za kielimu badala yake
inaweza kuzisaidia katika kuondokana na changamoto hizo.
Taasisi
ya International Language Training Centre inajihusisha na uendelezaji
wa lugha mbalimbali ikiwemo lugha za asili, Kiswahili, kiingereza,
kifaransa na nyinginezo.
Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments:
Post a Comment