MKAPA FOUNDATION YAKABIDHI NYUMBA 28, MAJENGO MAWILI YA UPASUAJI MKOANI SIMIYU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(wa tatu kulia) akikata utepe katika ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto) akisoma Jiwe la ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(wa pili kulia) akikagua baadhi ya vifaa tiba mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(kushoto) akisaini vitabu vya wageni mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ufunguzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, (kulia)Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation,Dkt.Hellen Mkondya Senkoro akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Ngulyati lililokabidhiwa kwa Serikali na Taasisi hiyo.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Bariadi,Mkoa wa Simiyu na Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation mara baada ufunguzi wa Jengo la Upasuaji (pichani) katika Kituo cha Afya.
Na Stella Kalinga
Taasisi
ya Benjamin Mkapa Foundation imekabidhi Serikali jumla ya Nyumba 28
kati ya 48 zinazotarajiwa kujengwa kwa ajili ya watumishi wa Idara ya
Afya na Majengo Mawili ya Upasuaji kwa ajili ya huduma za akina mama
wajawazito Mkoani Simiyu.
Akipokea
na kufungua Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya cha Ngulyati
Wilayani Bariadi na Nyumba za Watumishi katika Hospitali ya Mkula
wilayani Busega, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto , Mhe.Ummy Mwalimu ameishukuru Taasisi hiyo kwa kuuunga mkono
Serikali katika uboreshaji wa huduma za Afya, hasa katika ujenzi wa
miundombinu ya Afya.
Mhe.Waziri
amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuboresha huduma za Afya
kwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, miundombinu
ya Afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati
na Majengo ya Upasuaji, hivyo upatikanaji wa majengo hayo utasaidia
wananchi wa maeneo husika kupata huduma zinazotakiwa.
Mhe.Waziri
ameongeza kuwa Serikali imeanza kwa kuboresha upatikanaji wa dawa na
vifaa tiba kwa kuongeza bajeti, ambapo kwa Mwaka 2015 zilitengwa jumla
ya shilingi bilioni 31 na mwaka 2016 zimetengwa shilingi bilioni 51.
Amesema
Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine imejipanga kujenga kiwanda
cha kutengeneza dawa Mkoani Simiyu, hivyo pindi kiwanda hicho
kitakapokamilika dawa za Vituo Mbalimbali vya kutolea huduma za Afya
zitanunuliwa Simiyu.
Aidha,
Mhe.Ummy Mwalimu ameutaka Uongozi wa Mkoa uhakikishe unasimamia
ukusanyaji wa mapato katika Vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, ili
sehemu ya mapato hayo itumike kununulia dawa na vifaa tiba kwa lengo la
kuwahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma bora za afya.
Katika
kukabiliana na tatizo la vifo vya akina mama wajawazito na watoto
wakati wa kujifungua, Mhe.Ummy Mwalimu amewataka akina mama wajawazito
kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya, ikiwa ni pamoja na
kituo cha Afya cha Ngulyati mahali ambapo Jengo la Upasuaji na wodi kwa
ajili ya akina mama wajawazito vimejengwa.
Sanjari
na hilo Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza kwa nyakati tofauti na wakazi wa
Ngulyati wilayani Bariadi na Mkula wilayani Busega, amewahakikishia kuwa
Wizara yake italeta watumishi wa idara ya afya ili kukabiliana na
upungufu uliopo na akazitaka Halmashauri zote mkoani Simiyu kutengeneza
mazingira mazuri ambayo yatawapa motisha watumishi watakaoletwa na
kuendelea kubaki Simiyu.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya nyumba za watumishi na majengo ya Upasuaji,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt.Hellen
Mkondya Senkoro amesema, Taasisi hiyo imekamilisha majengo hayo yote na
akaiomba Serikali kuweka miundombinu iliyosalia kama maji, vifaa vya
kutolea huduma na watumishi ili wananchi waweze kunufaika na miradi
hiyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishukuru
Taasisi ya Mkapa Foundation na akaahidi kuwa Serikali itajitahidi
kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa katika miradi ya Benjamin Mkapa
Foundation ili itekelezwe kwa tija na manufaa kwa wananchi.
Aidha,Mkuu
huyo wa Mkoa amemshukuru Waziri wa Afya,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee
na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kwa kutoa magari ya kubebea wagonjwa
(Ambulance) nane(08) kwa Vituo vya Afya,Hospitali za Wilaya na Hosptali
Teule ya Mkoa kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma.
Wakati
huo huo Mbunge wa Busega,Mhe.Dkt.Raphael Chegeni amemshukuru Mhe Waziri
kwa jitihada zinazoendelea kufanyika katika kuboresha huduma za Afya
Mkoani Simiyu na akamuomba aupe kipaumbele Mkoa wa Simiyu, hususani
Wilaya za Busega na Itilima ambazo ni mpya kila Wizara yake inapogawa
rasilimali au miundombinu mingine ya Afya.
Wilaya
za Mkoa wa Simiyu zilizonufaika na Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya
Upasuaji sambamba na wodi ya wazazi Bariadi na Busega ambayo yamejengwa
kwa thamani ya shilingi milioni 435, kwa upande wa Nyumba za Watumishi
wilaya ya Busega (Nyumba 10),Itilima (Nyumba 10) na Bariadi ni Nyumba 08
ambazo zimegharimu jumla ya shilingi bilioni 1.47.
No comments:
Post a Comment