WAFANYAKAZI WA AIRTEL WASHEREHEKEA SIKU YA WANAFAMILIA WET N WILD KUNDUCHI.
Watoto
wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia
ndani ya bwawa la kuogelea katika shamrashamra za siku ya wanafamilia
wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Afisa
Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara wa Kampuni ya Simu za Mkononi
YA Airtel (kulia), akimpa zawadi Beatrice Nalingigwa baada ya kuibukas
kidedea katika shidano la kuogelea katika shamrashamra za siku ya
wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya wafanyakazi na familia zao wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel
wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao
ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya
Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mwanafamilia
wa Airtel akiwapa chakula watoto ikiwa ni ishara ya upendo ulio ndani
ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa
kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .
Ni
muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na kujumuika kwa
pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya
matunda waliyoyapata kwa mwa huu.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi
yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na
familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya
kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi
kuimarisha mshikamano miongoni mwao. "Umoja na mshikamano ni nyenzo
muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika
familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya
kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.
Zaidi
ya wafanyakazi na wanafamilia 600 walishiriki katika bonanza hilo na
kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba,
soka la baharini, wavu na kuogelea. Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.
No comments:
Post a Comment