ETIHAD YAANZISHA HUDUMA YA MALEZI KWA WATOTO NDANI YA NDEGE.
Kutoka
kushoto ni Meneja wa Huduma za wateja wa Etihad, Turky Alhammadi,
Makamu wa rais wa huduma za wateja Bw.Calum Laming na Makamu wa Rais wa
Huduma na Mapokezi Sajida Ismail, wakikata keki katika sherehe za
uzinduzi wa vifaa vya michezo ya watoto na malezi.
Watoto wakifurahia katika sherehe za uzinduzi wa vifaa vya watoto zilizofanyika Abu Dhabi.
WAKATI
familia nyingi zikijiandaa kwa ajili ya kwenda mapumzikoni katika nchi
mbalimbali, Shirika la Ndege la Etihad limepiga hatua nyingine katika
ubunifu kwa kuajiri wasaidizi watakaosaidia kulea watoto ndani ya ndege
na kuweka vifaa maalumu vya michezo ya watoto wakati wote watakapokuwa
safarini.
Mkusanyiko
wa vifaa vya watoto ni huduma mpya katika shirika hilo, vifaa hivyo
vitakavyojumuisha vitafunwa na michezo mbalimbali ya watoto vinalenga
kuwaburudisha watoto watakapokuwa ndani ya ndege.
Vifaa
hivyo, vimezinduliwa katika sherehe ya watoto ilioyofanyika kwenye Chuo
cha Mafunzo ya Sanaa na Uvumbuzi cha Shirika hilo mjini Abu Dhabi.
Katika
ndege zinazoingia Abu Dhabi, kutakuwa na vifaa vya michezo kwa watoto
wenye umri wa miaka mitatu hadi miaka minane. Katika umri huo, vifaa
hivyo vitajumuisha vijitabu vidogo, kalamu za rangi, karata na sura za
bandia zenye rangi mbalimbali. Ndege zinakazotoka Abu Dhabi zitakuwa na
sanduku maalumu la michezo hiyo litakaloongezwa vionjo zaidi.
Watoto
wenye miaka 9-13 watakuwa na michezo ya rika lao kama vile; Chemsha
bongo na uundaji wa maumbo mbalimbali, pia kutakuwa na makasha maalumu
ya Abu Dhabi yenye kalamu rula, peni na vitabu vya nukuu.
Watoto
wanaopenda michezo ya kompyuta na teknolojia pia watapata nafasi ya
kufurahia filamu mbalimbali, vipindi vya runinga na programu za kisasa
katika vifaa vya kidigitali na watakaosafiri umbali mrefu, watahudumiwa
na wasaidizi waliopitia mafunzo maalumu. Wasaidizi hao walianza rasmi
kuhudumu mwezi Septemba, 2013.
Makamu
wa Rais wa Huduma za Wageni katika Shirika la Etihad, Calum Laming
alisema: “Tunaelewa ugumu uliopo wakati wazazi wanaposafiri umbali
mrefu na watoto, hii ndio sababu iliyotufanya kuandaa mazingira rafiki
kwa watoto wanapokuwa safarini, pia ni sehemu ya juhudi zetu za
kuboresha huduma za anga hasa kwa wanaosafiri kifamilia na watoto
wadogo.”
Vifaa
vya watoto vimetengenezwa na kampuni inayotengeneza vifaa vya watoto ya
Milk Jnr’s & KidWorks iliyopo Uingereza, ambayo ni mshirika wa
kitengo cha Malezi ya Watoto- Etihad na Kitengo cha Maendeleo. Mradi huo
pia unahusisha wahusika wa michezo ya watoto kama Simba kundai, Nyuki
Zoe, Ngamia Jamool na Boo- Panda. Kampuni ya Milk Jnr’s & KidWorks
imechapisha nembo za watoto zenye maumbo mbalimbali yanayowakilisha
ardhi ya Abu Dhabi katika sare za wafanyakazi wa Etihad.
Katika kuboresha huduma zake, Etihad itazindua huduma mpya ya chakula kwa watoto Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi
wa huduma za wateja Zoe Telfer alisema: “Lengo la mradi huu ni kupata
suluhisho la changamoto ya kusafiri na watoto katika ndege zetu. Tunatoa
huduma hii kwa safari ndefu na safari zenye umbali mfupi huku
tukizingatia sifa za kipekee za Shirika letu.”
No comments:
Post a Comment