WAZIRI WA ARDHI WILLIAM LUKUVI AWAFUTIA HATI WALIOMIKISHWA ENEO LOTE LA MAKABURI YA KINYEREZI SOKONI
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akisalimia na DAS wa wilaya
ya Ilala Edward Mpogolo, alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya
Kinyerezi Sokoni, kufuatia mgogoro wa wananchi wawili kumilishwa eneo
hilo la makaburi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja.
Katika sakata hilo, Waziri Lukuvi ameagiza kufutwa kwa umiliki huo
mara moja ifikapo leo jioni, na pia kugiza kusakwa Pascal Kyonya Kazungu
na Ntitonda Chukilizo waliomilikishwa eneo hilo watafutwe na
kufikishwa ofisini kwake kesho.
Kadhalika amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam,
Leo Komba, kuorodhesha majina ya maofisa ardhi wote walioshiriki
kuwamilikisha ardhi hiyo ya eneo la makaburi ili aweze kuwashughulikia
kwa kuwachukulia hatua za kisheria.
Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kalua
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akipatiwa maelezo na Mbunge
wa Segerea Bona Kalua alipowasili kwenye eneo hilo la Makaburi ya
Kinyerezi Sokoni leo. Kushoto ni DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.
Waziri
Lukuvi akiwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine
alipowasili leo kutatua mgogoro wa kumilikishwa eneo la Makaburi ya
Kinyerezi Sokoni Dar es Salaam,.Kushoto ni Dar wa Wilaya ya Ilala,
Edward Mpogolo
Waziri Lukuvi akihoji jambo kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo
Waziri
Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi
alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo. Kulia ni
Mbunge wa Segerea Bona Kalua
Wananchi wa eneo la Kinyerezi Sokoni wakiwa wamemzunguka Waziri Lukuvi alipowasili kwenye eneo la Makaburi hayo leo
Kaimu
Mkurugenzi wa Ardhi jiji la Dar es Salaam, Leo Komba (kulia) akitoa
maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu anachofahamu juu ya wananchi wawili
kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo
"
Sasa hapo mimi sima la ziada, Wewe si ndiyo Mkurgenzi?" Sawa kuanzia
mda huu, nakuagiza ukafute umilikishwaji ardhi uliofanywa katika eneo la
makaburi haya", alisema Waziri Lukuvi na kuongeza " Na wale
waliomilikishwa hapa nitafutieni kesho waje kwangu wanieleze ilikuwaje
hata wakapata kumilikishwa eneo hili, na wale wote walioshiriki kwa
namna yoyote katika kufanya hili uniletee majina yao mara moja".
Diwani
wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine, akimshukuru Waziri wa Ardhi
Nyumba na Makazi, William Lukuvi baada ya kutoa uamuzi wa kufuta
umilikishwaji wa eneo hilo la makaburi kwa watu wawili.
Waziri
Lukuvi akifuatana na DAS wa wilaya ya Ilala wakati akiondoka kweneye
eneo hilo la makaburi ya Kinyerezi, ambako amefanikiwa kumaliza mgogoro
wa wananchi na watu wawili waliokuwa wamemikishwa eneo hilo la Makaburi
ya Kinyerezi Sokoni. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi Grayson
Celestine. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment