Header Ads

VIONGOZI WA CUF WAKIONGOZWA NA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD WAMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE MHE. JOB NDUGAI NYUMBANI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

 

post-feature-image

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

 Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam 
 Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee kuwa na afya njema ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Viongozi wa CUF wamefika nyumbani kwa Mhe. Spika, Job Ndugai kumjulia hali baada ya kurejea hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO

1 comment:

Anonymous said...

Сумки из кожи актуальны всегдаи к тожу же при правильном использовании сливаются практически с любой верхней. Кожаная сумка отличается долгим временем ношения и роскошным видом. При грамотном уходе сумочка из натурального природного вещества прослужит намного дольше, нежели из ситнетическогои к тому же с годами она, как хорошее вино, становится прекраснее, раскрывая свою истинную красоту. Отобрать сумку из кожи необходимо воспользовавшись магазином недорогие сумки интернет, так как там в наличии достаточно вариантов сумочек. На ресурсе вы обнаружите отзывы покупателей, которые помогут и сделать правильный выбор сумочки.

Powered by Blogger.