MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KATIKA KILELE CHA KIZIMKAZI DAY
Vijana wa Kiume wakishindana kukuna nazi ikiwa sehemu ya
mashindano ya Siku ya Kizimkazi (Kizimkazi Day).
Wakina Mama wakishindana kufunga kamba kwenye kilele cha
sherehe za Kizimkazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Kizimkazi Mkunguni kwenye
kilele cha Sherehe za Siku ya Kizimkazi ambapo wanakijiji hutumia siku hiyo
maalum kujadiliana mambo ya maendeleo na kushiriki michezo mbalimbali pamoja na
kula vyakula vya asili pamoja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka
kwa wakina mama wa kijiji cha Kizimkazi Mkunguni kwenye kilele cha sherehe za
Siku ya Kizimkazi
5. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Ndugu Idrisa
Kitwana wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Kimkazi (Kizimkaziday) kwenye
kijiji cha Kizimkazi Mkunguni. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment