BREAKING NEWZ....MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII MKOANI SIMIYU, BUNAMHALA, RAMADHANI SAID ASIMAMISHWA KAZI LEO MKOANI SIMIYU.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya
amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii
Bunamhala, Bw. Ramadhani Said kilichopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi
Mkoani Simiyu, kutokana na utendaji usioridhisha na kumteua Bi. Levina
Mrema kushikilia wadhifa huo.
Naibu
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya
(kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii
Bi. Levina Mrema (kulia) aliyemteua wakati alipokuwa katika ziara yake
ya siku moja Mkoani Simiyu.
Aliyekuwa
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Bunamhala Ramadhani Saidi
(Aliyesimama) akitoa maelezo juu ya chuo hicho kwa Naibu Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (hayupo pichani) wakati
wa ziara yake.
No comments:
Post a Comment