Watuhumiwa dawa za kulevya wazidi kubanwa
WAZIRI
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa
amemtaka Mkuu wa Magereza mkoa wa Lindi, kuhakikisha hakuna mtuhumiwa wa
dawa za kulevya atakayetoweka katika gereza la mkoa huo.
Amesema
kuna watuhumiwa wa dawa za kulevya ambao wanahifadhiwa katika gereza la
mkoa wa Lindi hivyo ni vema akajiridhisha kama ulinzi na usalama wa
watuhumiwa hao umeimarishwa.Hata hivyo, Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka
mkuu wa gereza hilo kuwa makini na baadhi ya zabuni wanazozitoa kutoka
nje na kuhakikisha ulinzi unaimarisha wakati wote gerezani hapo.
Waziri
Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo jana (10 Aprili, 2016) wilayani Ruangwa
wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Lindi iliyowasilishwa
kwake na Mkuu wa mkoa huo, Godfrey Zambi.“Mkuu wa Magereza wa mkoa
atembee gereza ambalo wanashikiliwa watuhumiwa wa dawa za kulevya na
aangalie mradi unaolenga kupeleka maji gerezani hapo kama ni kweli au
njia…,” amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.
Aidha,
Waziri Mkuu, Majaliwa amemtaka mkuu huyo wa Magereza kujiridhisha kama
ulinzi na usalama wao umeimarishwa na kuhakikisha hakuna mtuhumiwa
anayetoweka.Awali akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu, mkuu wa mkoa wa
Lindi, Zambi amesema matumizi ya dawa za kulevya hususan kwa vijana ni
miongoni mwa changamoto zinazoukabili mkoa huu ambapo wilaya ya Kilwa
inaongoza kwa kuwa na waathirika wengi.
Amesema
matumizi ya dawa hizo yanasababisha kupunguza kwa nguvu kazi kwani
watumiaji wengi ni vijana, hivyo alitoa wito kwa wananchi kushirikiana
na serikali katika kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwa kuwafichua
wauzaji na watumiaji.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment