BAYPORT YAKABIDHI HATI ZA VIWANJA VYA VIKURUTI.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI
ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo
imekabidhi hati za viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani
kwa baadhi ya wateja waliomaliza kulipa mikopo yao tangu walipochukua
mikopo hiyo yaa viwanja mapema mwaka jana.
Baadhi
ya wateja waliokabidhiwa hati hizo ni pamoja na Desidery Didas
Kalimwenjuma wa Temeke na James Moses Lubinza wa Kimara jijini Dar es
Salaam, huku hati za wateja wengine zikiwa zimekaamilika kwa ajili ya
kukabidhiwa wateja hao ambao walikuwa miongoni mwa Watanzania
waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, vilivyokuwa
vinauzwa na Bayport kwa kushirikiana na Kampuni ya Property
International Ltd.
Afisa
Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed (kushoto),
akishuhudia bwana James Moses Lubinza akitia sahihi katika tukio la
upewaji wa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha,
mkoani Pwani leo mchana, jijini Dar es Salaam. Lubinza alikuwa miongoni
mwa Watanzania waliochangamkia fursa ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
Huduma hizo za viwanja mwaka huu zinaendelea kwa kuanzishwa miradi ya
Bagamoyo, Kigaamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa vikuhusisha watumishi wa
umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Picha kwa hisani
ya Bayport Financial Services.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services Ngula Cheyo
katikati akikabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti kwa mteja wao James
Moses Lubinza leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Sheria wa
Bayport, Mrisho Mohamed.
Afisa
Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akiangalia
mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma wakati anatia sahihi katika
makabidhiano ya kupewa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani
Kibaha mkoani Pwani.
Afisa
Sheria wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akimkabidhi
hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma.
Mwanasheria
wa Bayport Financial Services Mrisho Mohamed kushoto akipiga picha ya
pamoja na mteja wao Desidery Didas Kalimwenjuma baada ya kumkabidhi hati
yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha mkoani Pwani leo mchana.
Akizungumza
leo mchana katika makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko
na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema ni furaha yao kubwa
kuanza kutoa hati ya viwanja vilivyouzwa kwa baadhi ya Watanzania
walioamua kuchangamkia fursa za viwanja vyao. Alisema hatua hiyo ni
sehemu muafaka ya kuhakikisha kwamba viwanja hivyo vilivyopimwa na
vyenye hati vinakuwa sehemu ya kuendeleza na kusaidia wananchi ambao kwa
kupitia viwanja hivyo wanaweza kuvitumia katika fursa mbalimbali kama
vile mikopo, kujenga nyumba za biashara na makazi ya kuishi wao na
familia zao.
“Hii
ni hatua muhimu kwetu Batyport kuona viwanja vya Vikuruti vimeanza
kutoka kwa hati zao na kuona kila aliyepata kiwanja basi hatakuwa na
usumbufu wowote wa kupewa hati yake, iwe kwenye mradi wa Vikuruti au
maeneo mengine ya Tanzania tunayoendelea na biashara ya kuuza viwanja
kwa njia ya fedha taslimu na mkopo.
“Tunawahakikishia
usalama na huduma bora kabisa kutoka kwetu Bayport, tukiamini kwamba
viwanja vyenye hati tunavyotoa ni maeneo mazuri na yanayoweza kujibu
maswali rahisi ya Watanzania wote kuweza kumiliki ardhi kwa utaratibu
rahisi na mzuri,” alisema Cheyo.
Akizungumza
baada ya kupewa hati yake, Kalimwenjuma alisema anashukuru kwa kupata
hati yake haraka bila usumbufu wowote, hali inayoonyesha umakini mkubwa
uliokuwapo kwenye huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
“Nashukuru kwa sababu nilikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza
kununua viwanja vya Bayport na leo nimepigiwa simu kwa ajili ya
kukabidhiwa hati yangu huku nikiwa na furaha kubwa pamoja nja
kuwapongeza mno kwa huduma bora,” Alisema.
Naye
Lubinza alisema hajawahi kukutana na huduma bora za viwanja kama vya
Bayport kwa sababu havina longolongo wala usumbufu wowote, jambo
linaloonyesha utulivu na umakini uliozalisha kupewa hati yake haraka
bila tatizo. “Ni maendeleo makubwa kwa kuwekeza fedha zangu kwa kununua
viwanja vya Vikuruti nikiamini kuwa ardhi ni kitu kinachopanda thamani
siku hadi siku, huku nikifurahia zaidi kwa sababu ni miongoni mwa
Watanzania waliopewa hati na Bayport,” Alisema.
Maeneo
mengine ya Tanzania ambayo Bayport inatoa mikopo ya viwanja ni pamoja
na Bagamoyo (Kimara Ng’ombe), Kibaha (Boko Timiza), Kilwa (Msakasa),
Kigamboni (Tundi Songani) na Chalinze katika maeneo ya (Kibiki na
Mpera), ambayo Watanzania wote wakiwamo watumishi wa umma, wafanyakazi
wa kampuni binafsi na wajasiriamali wanaweza kupata fursa ya kukopeshwa
viwanja hivyo vilivyopimwa na vyenye hati na kuidhinishwa na mamlaka
zote za Serikali kupitia kwa wabia wao wa kibiashara.
Kwa
viwanja vinavyoendelea kukopeshwa, wilayani Kilwa eneo la Msakasa
kilomita moja ya mraba inauzwa kwa Sh 2000, Chalinze ni Sh 4500,
Bagamoyo Sh 10,000, Kigamboni Sh 10,000 na Kibaha mkoani Pwani mita ya
mraba itapatikana kwa Sh 9000.
No comments:
Post a Comment