PPF WAKABIDHIWA RASMI JENGO JIPYA LA KISASA WALILOJENGA JIJINI ARUSHA LENYE THAMANI YA BILIONI 32.5
Kiongozi
Mkuu wa mfuko wa PPF (Director General) William Erio (kushoto) akipokea
michoro ya jengo jipya la PPF Jijini Arusha kutoka kwa Mbunifu na
Msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Arch. Dudley Mawalla
(kulia) kutoka kampuni ya MD Consultancy Ltd ya Dar es Salaam, katika
hafla fupi ya makabidhiano rasmi ya jengo kutoka kwa mkadarasi wa
kichina CREJ (EA) Ltd. Anayeshuhudia Katikati ni Injinia wa Miradi ya
PPF, Injinia Marko Kapinga.
DG
William Erio (pichani juu) ameisifu timu yote iliyoshiriki kufanikisha
kukamilika kwa mradi huo katika ubora uliotakiwa na katika bajeti
iliyopangwa mwaka 2012 bila kuongezeka pesa yoyote, kuanzia kitengo cha
miradi ya PPF makao makuu, wabunifu na wasimamizi, mamlaka za Jiji,
idara nyingine za Serikali na wakandarasi wenyewe.
Jengo
hilo maalumu kwa shughuli za ofisi na biashara lenye ghorofa 10 sambamba
na eneo la basmenet yenye uwezo wa kupaki magari 168, lina thamani ya
shilingi bilioni 32.5. Limejengwa eneo la Corridor, Kitalu Na. 15
Barabara ya zamani ya Old Moshi Jijini Arusha. lina huduma zote muhimu
kwa majengo ya kisasa zikiwemo 'lifti' za kutosha, majenereta makubwa,
mataki ya maji na mafuta ya jenerato, mfumo wa kukabiliana na moto na
bila kusahau camera 90 za usalama na eneo kubwa la kuegesha magari ndani
ya jengo.
Kwa
mujibu wa Mbunifu na Msimamizi Mkuu wa mradi huo wa kisasa, Arch Mawala,
ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi Agosti 2 mwaka 2018 ukitarajiwa
kukamilika miezi 104 baadae na ulikamilika rasmi (practica completion)
mwishoni mwa mwezi Disemba mwakaa jana. Hata hivyo imewachukua miaka
miwili na miezi 3 kuweza kukamilisha kila kitu katika ubora wa kiwango
cha juu, ambapo miezi hiyo mitatu ni ya ngongeza ya muda kutokana na
sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.
Sehemu ya muonekano wa mbele wa jengo
Mpaka
kufikia kukabidhiwa kwake hii leo, tayari ukaguzi wa mamlaka za Jiji na
Usalama wa Majengo umeshakamilika na ruhusa ya matumizi kutolewa. Tayari
jengo hilo limeshapata wapangaji watatu ambao wapo kwenye jengo tayari
zikiwemo benki za TIB na FBNB, huku asilimia 21 ya wapangaji wengine
wakiwa wamekwisha saini mikataba na PPF na wapangaji wengine 24 wakiwa
katika mazungumzo.
Aidha
kwa maelezo ya Mratibu wa PPF Kanda ya Kasakazini, Bw Onesmo Rushahi,
Ofisi za Kanda ambazo kwa sasa ziko maeneo ya Kaloleni Jijini hapa
zitahamishiwa katika Jengo hili jipya, huku mkakati wa PPF ukiwa ni
kuhakikisha baada ya mwaka mmoja jengo hilo liwe limefanikiwa kupata
wapangaji maeneo yote kwa shughuli za ofisi na biashara.
Mkandarasi
Mkuu ni kampuni ya CRJE (EA) Ltd akisaidiwa na wakandarasi wengine kwa
huduma za jengo kama vile ICT na Usalama - SSTL Group Ltd, Lifti - S.E.C
(EA) Ltd, AC - M.A.K Enginering Co. Ltd, Mfumo wa maji safi na maji
taka - Jandu Plumbers Ltd, na Umeme ni Central Electrical International
Ltd. Pia kulikuwa na mamlaka za kiserikali kama wasimamizi wa usalama
makazini OSHA, Idara ya maji Asurha - AUWSA, NAESCO, Halmashauri ya Jiji
na Bodi za Ukaguzi kama AQRB na CRB.
No comments:
Post a Comment