ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016".
Mrimbwende
Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss
Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.
Miss
Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika
Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa
ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii
ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza
kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.
Mashindano
hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika
Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es
Salaam.Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha
kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini,
Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata
Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.
Wshiriki
Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano
ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17),
Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18),
Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.
Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu
Kampuni
ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni
yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick
Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja
zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa
Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili
simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya
B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu
Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa
katika picha ya Pamoja na washindi.
No comments:
Post a Comment