Ofisi ya Rais-UTUMISHI yaendelea na Vikao kazi kwa Njia ya Video (Video Conference).
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Laurean Ndumbaro (picha ndogo kulia)
akiongoza kikao kazi kwa njia ya video kilichohusisha Ofisi ya
Rais-Utumishi,Ofisi ya Rais- TAMISEMI,Wizara ya Fedha,Wizara ya Viwanda,
Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wakala ya Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na
ofisi za Sekretarieti za mikoa ya Iringa, Pwani, Mtwara, Dar es Salaam,
Kagera,Kigoma.
Mkurugenzi
Msaidizi kutoka Idara ya Ushauri na Uchambuzi Kazi Ofisi ya
Rais-UTUMISHI Bi.Sakina Mwinyimkuu (kushoto) akiwasilisha mada kuhusu
Uimarishaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini Serikalini kwenye kikao
kazi kwa njia ya video kilichofanyika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa
Njia ya Mtandao (TaGLA).
Washiriki wa kikao kazi kwa njia ya video wakimsikiliza mtoa mada.
No comments:
Post a Comment