MGAMBO WASIO WAADILIFU KUSHUGHULIKIWA.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kutokana
na tabia ya baadhi ya mgambo katika Halmashauri za Jijini la Dar es
Salaam kujipatia fedha kwa njia zisizo za halali, serikali kupitia
Halmashauri zake imejipanga kuwachukulia hatua za kisheria migambo wote
watakaobainika kujishirikisha na vitendo vya rushwa.
Akitoa
ufafanuzi juu ya madai ya wanachi juu ya mgambo wanaochukua rushwa nje
ya faini halali zinazistahili kutozwa katika Halmashauri ya Manispaa ya
Wilaya ya Ilala, Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shabibu amesema
kuwa zipo baadhi ya taarifa wamepewa na watawachukulia hatua kwa
kuwasitishia mikataba wale wote watakaobainika kukiuka sheria na
taratibu za kazi.
“ Wapo
mgambo ambao watumia vitambulisho feki na kufanya vitendo vya rushwa
bado hatujawakamata ila hatutawafumbia macho tutawachukulia hatua kali
za kisheria kwa yoyote atakayekamatwa akipokea rushwa na hata wale
watakaotoa rushwa”
“Napenda
kuwaasa watanzania kuacha kuwapa fedha mgambo ili kukwepa kulipa faini
halali hivyo basi nawaasa watu kutii Sheria bila shuruti kama umefanya
kosa kwa mujibu wa Sheria lipa faini kwa mujibu wa Sheria lipa faini
halali ili tuondoe vitendo vya rushwa na kuiongezea mapato Serikali
”Alisema Tabu.
Afisa
Tabu amewaomba watanzania kutoa taarifa za mgambo wote wanaopokea rushwa
na kusisitiza kuwa tabia hii inayoendelea ikome mara moja na mgambo
wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa watasitishiwa
mikataba yao ya kazi kwa kukiuka maadili ya kazi zao
Mgambo
katika Jiji la Dar es Salaam wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuchukua
rushwa kuanzia shilingi 5,000/= mpaka 10,000/= badala ya kutoza faini ya
shilling 50,000/= inayostahili kutoza kwa wale wanaokiuka kanuni na
taratibu za afya na mazingira katika Halmashauri mbalimbali.
Katika
kupambana na suala la mgambo wasio waadilifu,Halmashauri zimejipanga
kuwaajiri vijana walipitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
waliopata mafunzo yenye yenye kujenga uadili na uwajibikaji katika kazi
ili kudhibiti suala la mmomonyoko wa maadili na utendaji kazi mbovu wa
mgambo katika Halmashauri mbalimbali.
No comments:
Post a Comment