MBUNGE WA ISMANI WILIAM LUKUVI ATOA MSAADA WA FEDHA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IDODI
Mbunge
wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa Ardhi
,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa
kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha kiasi cha Tsh milioni 2
za kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi watakaohamishiwa makazi mapya
kutoka kitongoji cha Kitanewa Idodi ambao nyumba zao zilisombwa na
mafuriko .
MKazi wa kitanewa Idodi akimpongeza mbunge wake Lukuvi kwa kuwajali wananchi
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Katikati na kamati yake ya Ulinzi
na usalama wakitazama daraja la Iringa -kuelekea hifadhi ya Ruaha ambalo
awali lilikuwa halipitiki baada ya kusombwa na mafuriko na sasa
linapitika
Wananchi
wanaotakiwa kuhamishwa kwenda makazi mapya baada ya nyumba zao
kusombwa na mafuriko wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Lukuvi .
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi amewapa pole waathirika wa
mafuriko wa kata ya Mapogolo tarafa ya Idodi wilaya ya Iringa mkoani
Iringa kwa kuwakabidhi msaada wa pesa zaidi ya Tsh milioni 9 kwa ajili
ya kusaidia mahitaji mbali mbali ikiwa ni pamoja na kurejesha miundo
mbinu ya maji safi iliyoharibiwa na mafuriko.
Bw
Lukuvi ambae pia ni waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi
alikabidhi msaada huo jana baada ya kutembelea waathirika hao waliopo
kambi ya Kitanewa pamoja na kutembelea eneo la barabara ya kutoka Iringa
kuelekea hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo kwa sasa imekarabatiwa baada
ya awali barabara hiyo kukatika kutokana na mafuriko hayo , alisema kuwa
lengo lake kama mbunge wa jimbo hilo la Isimani na serikali ni kuona
wananchi waliokumbwa na mafuriko wanaendelea kusaidiwa .
Alisema
kuwa awali aliomba msaada wa mahindi tani 100 kutoka serikali kwa ajili
ya waathirika hao wa mafuriko Idodi na Pawaga ikiwa ni pamoja na
kuwasaidia msaada wa fedha kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya
kuwawezesha waathirika hao wa mafuriko kupata mahitaji mengine kama
mboga na pesa ya kusagia mahindi hayo .
Bw
Lukuvi alisema kuwa kwa ajili ya kurejesha huduma ya maji kijijini hapo
amewasaidia kiasi cha Tsh miliobni 4 ambazo wameomba kwa ajili ya
kuboresha miundo mbinu hiyo ,pia kiasi cha Tsh milioni 2 kwa ajili ya
kukiwezesha kijiji kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi waliotoa ardhi yao
kwa ajili ya wakazi wa kitongoji cha Kitanewa ambao wanapaswa
kuhamishwa eneo hilo la mafuriko la kupewa makazi mapya.
"
Waambieni watu wenye mashamba ambayo yatachukuliwa kwa ajili ya viwanja
mwaka huu wavune mazao yao na baada ya hapo kila mmoja muweze kumlipa
fidia ya Tsh 200,000 na baada ya hapo waitini wataalamu wa ardhi ili
waweze kupima viwanja na mpanfgilio mzuri zaidi kwa ajili ya makazi
mapya,pia nataka hata mashamba ya kawaida ya wananchi kupimwa ili kupata
hati za ardhi zitakazowawezesha kutumia kupata mikopo ....ila
nitawaletea mashine za kufyatulia tofari ambazo unaweza kuzijengea bila
kuchoma "
Alisema
kuwa kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa nyumba bora mwananchi
atakayekuwa wa kwanza kupandisha jengo atamchangia bati japo kwa sasa
amekwisha toa bati zaidi ya 300 kwa mkuu wa wilaya ya Iringa kwa ajili
ya waathirika hao.
Bw
Lukuvi pia amewapongeza wadau mbali mbali zikiwemo taasisi za dini ,watu
binafsi ,taasisi ya kifedha pamoja na mifuko ya hifadhi za jamii kwa
kujitolea misaada mbali mbali kwa ajili ya waathirika wa mafuriko na
wagonjwa wa Kipindupindu Pawaga .
Pamoja
na kuwashukuru wadau hao Lukuvi alimpongeza waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kwa kuwatembelea waathirika hao wa Mafuriko na wale wa Kipindupindu
Pawaga .
Hata
hivyo Lukuvi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na
viongozi wote akiwemo mkuu wa mkoa Amina Masenza kwa kusimamia shughuli
mbali mbali ikiwemo ya urejeshaji wa miundo mbinu ya barabara iliyokuwa
imekatika katika barabara ya Iringa - Ruaha .
Katika
hatua nyingine Bw Lukuvi aliagiza serikali ya kijiji cha Mapogolo
kutowabagua wananchi katika kugawa chakula hicho cha msaada na kutaka
hata ambao si waathirika wa mafuriko ambao wana njaa wapewe chakula
hicho cha msaada kwa waathirika wa mafuriko .
Wakati
huo huo Waziri Lukuvi alisema kuwa serikali inakusudia kuijenga
barabara ya Iringa- kuelekea hifadhi ya Ruaha kwa kiwango cha lami kama
mbavyo Rais Dr John Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni kupitia ilani
ya uchaguzi ya CCM
Pia
kwa ajili ya kuwafanya wananchi kunufaika watalii wanaotembelea hifadhi
hiyo ya Ruaha Iringa alisema tayari jitihada za kujenga viwanja vidogo
vya ndege nje ya hifadhi ya Ruaha zimeanza na kuwa lengo la serikali ni
kuwahamisha wafanyakazi wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo na kujumuika na
wananchi nje ya hifadhi ili waweze kupata mahitaji kama wananchi
wengine.
No comments:
Post a Comment