Jengo la posta lateketea kwa moto

JENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma jana limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa.
Akizungumzia
kutekeleza kwa jengo hilo Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Magreth
Mlyomi alisema mpaka sasa kuna hasara kubwa kutokana na kutekeleza jengo
hilo sambamba na vifaa vyote vya ofisi.Mlyomi alisema licha ya kuwa
hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepoteza maisha katika jengo hilo lakini
mpaka sasa kuna vitendea kazi vingi vya ofisi pamoja na mizigo ya
wateja imeteketea.
“Kuna
mizigo mingi pamoja na vifaa vya kazi vyote vimeteketezwa na moto na kwa
taarifa nilizopata kulikuwa na mizigo ya watu, inaonesha kuwa chanzo
cha moto ni umeme,” alieleza Meneja huyo.Akizungumzia kuhusu masuala ya
miundombinu ya maeneo husika alisema ni mibovu na kutokana na changamoto
hiyo suala hilo lipo katika mamlaka husika ya manispaa.
Kwa
upande wake katibu wa wafanyabiashara katika soko la Sabasaba katika
Manispaa ya Dodoma, Gergod Lugusi alisema jana saa nne asubuhi kulitokea
moto mkali ambao uliunguza jengo hilo.
Alisema
chanzo cha moto huo inasemakana kuwa ni tatizo la umeme na uongozi
ulilazimika kutoa taarifa katika kikosi cha zima moto na bila kuchelewa
walifika kwa wakati.Hata hivyo alisema licha ya kufika kwa wakati katika
tukio bado kikosi hicho kilikutana na kikwazo kwa kutokana na
miundombinu kuwa mibovu na migumu kupitika
No comments:
Post a Comment