WAZIRI KITWANGA AKABIDHI VITANDA, MAGODORO, MASHUKA JIMBONI KWAKE, AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MAJI NA BARABARA MISUNGWI
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya
cha Misasi, Ernest Msiba akikijaribu kimoja kati ya vitanda 20 kabla ya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (watatu kushoto) kumkabidhi
vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Nathan
Mshana (wapili kushoto). Waziri Kitwanga alikabidhi vitanda (20),
magodoro (20) pamoja na shuka (20) kwa ajili ya Kituo cha Afya cha
Misasi pamoja na vitanda sita kati ya hivyo walikabidhiwa Zanahati ya
Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo. Hafla ya makabidhiano
hayo ilifanyika katika Kijiji cha Misasi. Kushoto kwa Waziri ni Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, ambapo
shirika lake pia lilitoa baadhi ya misaada katika kituo hicho cha afya. Picha zote na Felix Mwagara.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa
PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani
Mwanza, Charles Kitwanga, magaodoro (20) na shuka (20) vyenye thamani ya
shilingi milioni tatu na laki tano katika hafla iliyofanyika Viwanja
vya Kituo cha Afya Misasi, wilayani Misungwi. Waziri Chikawe baada ya
kukabidhiwa vifaa hivyo alivikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Misungwi, pamoja na vitanda (20) vyenye thamani ya Shilingi
milioni 16 ili aweze kuvigawa kwa Kituo cha Afya cha Misasi pamoja na
Zahanati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akikata utepe wakati akifungua jiwe la msingi la ujenzi wa
Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, jimboni humo
wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na
kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. Waziri Chikawe katika hotuba yake,
aliwaahidi wananchi wa eneo hilo upatikanaji wa maji hivi karibuni kwani
eneo hilo linamradi mkubwa wa maji wa Mamlaka wa Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA), hivyo ni lazima maji yasambazwe
kwa vijiji vyote vya jirani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi ya
Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, Wilaya ya Misungwi. Shule hiyo
inajengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na kuchangiwa na Mamlaka wa Maji
Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) ambayo inamradi
mkubwa wa maji katika Kijiji cha Ihelele ambapo shule hiyo inapojengwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Misasi mara baada ya
kukabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) katika Kituo
cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Waziri Chikawe katika hotuba yake
aliwaahidi wananchi wa eneo hilo ujenzi wa barabara ya lami pamoja na
upatikanaji wa maji.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Misungwi
(OCD), Sylivester Ibrahim akijibu maswali ya wananchi wa Kata ya Misasi
kuhusu usalama katika eneo lao. Ofisa huyo wa Polisi alipewa nafasi na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa) baada ya
wananchi hao kutaka kujua masuala ya haki zao waendapo Kituo cha Polisi
kuripoti matukio mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles
Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi
misaada mbalimbali ikiwemo vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka
(20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment