Header Ads

CHUO CHA KODI CHAIMARIKA KWA UMAHIRI WA MAFUNZO YA FORODHA NA KODI KIMATAIFA

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, Prof. Isaya Jairo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo picha) jijini Dar es Salaam juu ya Mahafali ya nane yatakayofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere tarehe 16 Januari mwaka huu, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Usimamizi wa Forodha na Kodi, Dkt. Lewis Ishemoi na  Bw. Charles Sabuni, Naibu mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala).
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna. --- Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii. CHUO cha Kodi kimeweza kupata hadhi kuwa kituo cha Umahiri wa Mafunzo ya Forodha na Kodi kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Issaya Jairo amesema wakati wakielekea katika mahafali ya nane chuo kimeweza kufikia hadhi hiyo. 

No comments:

Powered by Blogger.