MWAKA MWINGINE WA MAENDELEO MAKUBWA KWA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_M695OWfrS-pfCEsHQhz49Dvvg6W36HlCW-DBAoSLo2LXYUj_gNdpYWdNk7Vp9CpqF6mnY5ISDzgJ0eI59vj2a7auUR8zOIzCq9dc9rF6lBOcn9ahEUJgbeiAW8y2DvP5RmxRUr85kJJX/s640/Etihad_Airways_-_Airbus_A380-861.jpg)
SHIRIKA
la ndege la taifa la umoja wa falme za nchi za kiarabu la Etihad
limefurahishwa na ufanisi na utendaji wa operesheni zake kwa mwaka wa
2015 zilizowafanikisha kufikia malengo yao ya ukuaji ambapo sasa
wanabeba abiria wengi na mizigo mingi zaidi ya awali.
Mwaka
jana Shirika lilibeba abiria milioni 17.4, sawa na asilimia 17 zaidi ya
mwaka 2014, wakiendesha safari 97,400 za ndege zilizofikisha jumla ya
kilomita milioni 467.
Hii
ni dhahiri kwamba abiria walifurahia huduma hizi na hivyo uhitaji
uliongezeka, jambo ambalo lilisisitiza nguvu ya mikakati ya ukuaji
iliyowekwa na shirika la ndege la Etihad.
Kwa
ujumla, ndege za Etihad pekee zimebeba zaidi ya asilimia 75 ya abiria
waliosafiri kwenda na kuondokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu
Dhabi katika mwaka wa 2015. Etihad pamoja na washirika wake walio na
ndege zinazofika mji huo mkuu wa UAE wamefikisha jumla ya asilimia 84 ya
abiria waliotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.
James
Hogan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Etihad, alisema: “Katika mwaka
2015, tumeweza kuwapa mamilioni ya wasafiri chaguo lenye thamani ya
fedha katika usafiri wa anga na tumeleta nguvu mpya ya ushindani katika
sekta hii. Yote haya yametokana na huduma zetu zinazokidhi viwango vya
kimataifa ambazo pia zimejizolea tuzo mbalimbali. Pamoja na hayo,
mashirika mengi yanavutiwa kujiunga nasi na tunazidi kuongeza idadi ya
washirika wetu, kukuza ukubwa wa mitandao yetu ili kufika sehemu nyingi
zaidi duniani.
Hamna shirika lingine lenye kuleta tija na ushindani wa viwango hivi katika sekta hii”. Katika
mwaka 2015, Shirika la Etihad limezindua njia mpya kwenda Kolkata,
Madrid, Edinburgh, Entebbe, Hong Kong na Dar es Salaam, pamoja na huduma
ya moja kwa moja kwenda Brisbane.
Mwaka
jana pia Etihad walianza kutumia ndege aina ya Boeing 787-9 Dreamliner,
ambayo ilianza kutoa huduma za ndege za biashara kwenda Washington DC,
Zurich, Singapore na Brisbane. Mtandao wa ndege aina ya Airbus A380
umeongeza huduma zake za kuelekea London Heathrow na kuanza safari mpya
za kuelekea Sydney na New York.
Mwaka
huu, Shirika litaongeza safari zake za kwenda London Heathrow hadi
kufikia safari tatu kwa siku hii ni pamoja na mwanzo wa safari mpya za
ndege aina ya A380 kufika Mumbai na Melbourne, wakati Boeing 787 itaanza
kupaa kwenda vituo vipya vya Düsseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na
Johannesburg.
Etihad
pia iliongeza mizunguko katika njia za kusafiria 16 zinazotumika hivi
sasa ambazo hufika Bangkok, Chennai, Dammam, Delhi, Hong Kong,
Hyderabad, Istanbul, Jeddah, Kochi, Kozhikode, Melbourne, Mumbai,
Muscat, Seychelles, Tehran na Trivandrum.
Ili
kukabiliana na kasi ya ukuaji wake, Shirika la ndege la Etihad
liliongeza idadi ya washirika wake mwaka jana. Mkakati huu uliwapa fursa
abiria zaidi ya milioni tano kutumia ndege za Etihad, iliyosababisha
ongezeko la asilimia 43 ambayo ni abiria milioni 3.5 zaidi kuliko 2014.
Mkakati
mwingine ni makubaliano waliyozindua na Shirika la kimataifa la ndege
la Pakistan (PIA), wakati Etihad inaendelea kukuza na kuendeleza
ushirika wake na mashirika ya Air Serbia, American Airlines, flynas,
Jet Airways, Korean Air, NIKI and S7.
Kutokana
na hayo, Etihad sasa inawapa fursa abiria wake kuwa katika mtandao
utakaowawezesha kusafiri na kusafirisha mizigo kwenda sehemu 600 kwa
kuunganisha ndege na moja kati ya washirika wake 197 ama kusafiri na
washirika wake wa “codeshare” 49.
Mnamo
mwezi wa nne wa mwaka 2015, Shirika la ndege la Etihad lilipata kibali
kutoka kwa Ofisi ya Shirikisho la Usafiri wa Anga ya Uswisi (FOCA)
kukamilisha asilimia 33.3 ya uwekezaji katika shirika la ndege la
Darwin, ambazo ni ndege zinazoruka kanda za Uswisi.
Ndege
za shirika la Etihad ziliripoti kubeba tani 592,090 sawa na ongezeko la
asilimia 4 mwaka hadi mwaka. Mwaka jana, ndege hizi zimebeba asilimia
88 ya mizigo ya bidhaa kuingia na kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa
Abu Dhabi.
Katika
mwaka 2015, Etihad imefikisha mizigo vituo vipya sita duniani na sasa
huduma hii ya kusafirisha mizigo inapatikana katika jumla ya vituo 96
ambavyo hutumika na abiria wakati wa kusafiri. Shirika limepanua uwezo
wake wa kusafirisha mizigo kufika masoko mapya yakiwemo Dakar,
Nouakchott na Douala, ambapo imefanya jumla ya vituo vinavyosafirisha
mizigo tu kuwa 20.
Kufikia
mwisho wa mwaka 2015, Etihad ilifikisha jumla ya ndege 121 (ogezeko la
asilimia 9 mwaka hadi mwaka) yenye wastani ya umri wa miaka 5.8-
kulifanya kuwa shirika lenye ndege changa na zisizoharibu mazingira kati
ya wapinzani katika sekta nzima. Mwaka 2015 Shirika lilipokea Airbus 11
(A380 nne, A321 sita na A320 moja) na Boeing 787-9 Dreamliner nne huku
wakiongeza nafasi za kukodi pia.
Ili
kuunga mkono mikakati iliyojiwekea ya kukuza mtandao wao duniani,
shirika la Etihad litapokea ndege nyingine mwaka huu, zikiwemo Boeing
787-9 tano, A380 tatu na Boeing 777-200 Freighters mbili.
Bwana
Hogan alisema: “Tumeingia mwaka 2016 kwa kujiamini kwamba nguvu
tulizoonesha awali zitaendelea na zitatumika kuitambulisha Abu Dhabi
kama kitovu cha usafiri wa anga duniani.
“Tunaendelea
kukabiliana na changamoto, ikiwemo suala la ulinzi wa urithi wa
wasafirishaji wakubwa Marekani na Ulaya. Tunaendelea kuboresha huduma
zetu ili kuwahakikishia wasafiri wetu kwamba wanachagua kilicho bora
kati ya sisi na washindani wetu”.
No comments:
Post a Comment