WANAFUNZI 538 WATUNUKIWA VYETI VYAO KATIKA MAHAFALI YA NANE YA CHUO CHA TRA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.
WANAFUNZI
538 wa chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo
katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi.
Wameaswa hayo na Naibu
waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya nane
ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Nyerere.
amesema
kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu kwani
wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa.
Chuo
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko kibaha
mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani
chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.
Naibu
waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa
chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafali ya nane ya
chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere
leo jijini Dar es Salaam




No comments:
Post a Comment