BENKI YA WANAWAKE YATAKIWA KUWAWEZESHA KIUCHUMI NA KIELIMU WANAWAKE
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
wazee na watoto Ummy Mwalimu, ameitaka Bodi na Watendaji wa Benki ya Wanawake
Tanzania (TWB), kuhakikisha kuwa inawawezesha wanawake kiuchumi kwa kufikisha
huduma hiyo mbali zaidi ili kuifanya benki kuwa kimbilio la wanawake kweli .
Akizungumza katika ziara yake ya mafunzo
katika benki hiyo akifuatana na Naibu wake waziri Dakta HAMISI KIGWANGA, Katibu
mkuu na watendaji wa Wizara hiyo UMMY alisema wanawake wa Tanzania wanajitoa
sana katika kulea familia hivyo wakiwezeshwa watakuwa wamewezesha familia,
vijana na Taifa kwa ujumla.
Waziri huyo alisema watendaji wa benki hiyo ya wanapaswa kuweka
utaratibu mzuri wa utoaji wa huduma ambazo zitaweka fikra za wanawake pale
wanapotaka kuchukua mikopo au kuweka fedha zao katika benki kufikiria kwanza
benki ya TWB.
“Mimi huwa naona uwezeshaji wa kweli wa
wanawake ni kuhakikisha kuwa tunawawezesha kiuchumi na kielimu kwasababu
mwanamke atashiriki kulima kupanda lakini ikifika kuvuna tu mazao sio yake
hivyo endapo tutapata fedha zinazohusu mfuko wa wanawake Serikalini tutaomba
zipitishwe kwenye Benki ya Wanawake na tutakwenda kila Halmashauri kuanzisha
saccos za wanawake ili waweze kupata fedha za kukopeshwa na benki ya wanawake,’’alisema
Ummy.
No comments:
Post a Comment