Rais Mstaafu, Dk Ali Hassani Mwinyi atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA)
Rais Mstaafu wa Tanzania, MzeeAli
Hassani Mwinyi (katikati) akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa
Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) na Rais wa
Sudani ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho, Omar al-Bashir (wa pili kulia)
mjini Khartoum, Sudani hivi karibuni.
Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi
(wa pili kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa zamani wa Mahakama Kuu ya
Saudia, Abdulrahman Alsheikh Al Ashum alipotembelea Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Afrika (IUA) mjini Khartoum hivi karibuni na kutunukiwa
Shahada ya Heshima (PHD) ya Sayansi ya Jamii ya chuo hicho na Mkuu wa
chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Sudani, Omar al-Bashir. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Taasisi ya Munazzmat Al-Dawa wa Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Khalid A. Abdullah na kulia ni mke wa Mzee Mwinyi, Mama Khadija Mwinyi.
Rais Mstaafu, Ali
Hassani Mwinyi (katikati) akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosoma
katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) mjini Khartoum, Sudani
hivi karibuni
ambapo pia alitunukiwa Shahada ya Heshima (PHD) ya Udaktari wa Sayansi
ya Jamii ya chuo hicho na Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Rais wa
Sudani, Omar al-Bashir (hayupo pichani).
Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (wa pili kulia) akipokea nishati kutoka kwa Katibu Mkuu wa Taasisi ya Munazzmat
Al-Dawa, Abdulrahim Ali Ibrahim kutokana na mchango wa mzee Mwinyi
katika kusaidia mipango na shughuli za taasisi hiyo barani Afrika
hususani nchini Tanzania.
Rais mstaafu alitembelea nchini Sudani hivi karibuni ambapo akiwa huko
alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (PHD) ya Sayansi ya Jamii ya
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA). Kushoto ni Mkurugenzi wa
Taasisi ya Munazzmat
Al-Dawa wa Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Khalid A. Abdullah, Sheikh
Athumani Kaburu wa Tanzania na waalikwa wengine. (Picha na Peter Mgongo)
Rais Mstaafuwa Tanzania, Ali
Hassani Mwinyi (katikati) akilakiwa na wenyeji wake baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Khartoum nchini Sudani hivi karibuni ambako
pamoja na mambo mengine alitunukiwa shahada ya udaktari wa heshima ya
sayansi ya jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) kutokana
na mchango wake katika kusaidia maendeleo ya elimu nchini Tanzania na
Afrika.
No comments:
Post a Comment