MAADHIMISHO YA CCM KUFANYIKA ZANZIBAR KILELE KUITIKISA SINGIDA
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuadhimisha miaka 39 ya kuzaliwa kwake
na kumbukumbu hiyo itazinduliwa Januari 31,Unguja –Zanzibar chini ya
mgeni rasmi Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar Dk. Ali
Mohamed Shein.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati akitangaza maadhimisho ya chama
hicho,Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
amesema baada ya uzinduzi wa maadhimisho hayo Zanzibara,kilele chake
kitakuwa mkoani Singida ambako zitafanyika kazi mbalimbali ikiwemo na ya
kuingiza wanachama wapya, kufanya kazi za kujiletea maendeleo kwa
kujenga madarasa,kupanda miti,pamoja na kufanya kazi za usafi .
Amesema
viongozi wa kitaifa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu watapangiwa
shughuli za ujenzi wa chama na taifa kwa ujumla katika wilaya za Mkoa wa
Singida siku tatu kabla ya kilele ya maadhimisho ambayo yatafanyika
mkoani Singida.
Nape
amesema mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika
Februari 6 mkoani Singida,anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Chama
hicho,Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Dk.Jakaya Kikwete.
Kauli
Mbiu ya maadhimisho kwa Chama hicho kwa mwaka huu kimetajwa kuwa ni
“Sasa kazi,Kujenga Nchi na Kukijenga Chama”.Maadhimisho ya CCM
hufanyika kila Februari 5 ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa CCM
Februari 5 ,1977 iliyotokana kuungana kwa ASP na Tanu.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akizungumza na Baadhi ya
Waandishi wa habari,mapema leo kuhusiana na uzinduzi wa maadhimisho ya
sherehe za chama hicho pamoja na kilele chake ambacho kinatarajiwa
kufanyika mkoani Singida,Mkutano huo umefanyika kwenye ofisi ndogo za
chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba,jijini Dar .
No comments:
Post a Comment