Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw.
Nurdin Ndimbe (kushoto) akimkabidhi Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto
jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) msaada wa vyakula na
vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo.
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw.
Nurdin Ndimbe (kushoto) akishirikiana na Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya
Watoto jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) kupakua msaada
wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania
leo.
Afisa
Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan
Yahaya (kulia) akipakua msaada wa vyakula na vitu mbalimbali
vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe
Mkuu
wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw.
Nurdin Ndimbe (kushoto) akiagana na Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto
ya jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) mara baada ya kutoa
msaada wa vyakula na vitu mbalimbali.
(Na. Aron Msigwa- Dar es salaam)
Jamii
imeaswa kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu na makundi yenye mahitaji
maalumu hususan wafungwa walio magerezani na wasiojiweza ili kudumisha upendo na kuyafanya makundi hayo kujiona yanathaminiwa katika jamii.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es
salaam na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya
Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe wakati akikabidhi msaada wa vyakula na vitu
mbalimbali kwa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam vilivyotolewa
na Mahakama Kuu ya Tanzania kama zawadi yao ya mpya 2016.
Bw.
Ndimbe amesema Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa msaada wa vitu
mbalimbali vikiwemo Mchele, Sabuni, Vinywaji, Chumvi, Unga wa Ngano,
Unga wa Sembe, Mchele ,Sukari na Mafuta ya kupikia kwa Mahabusu hao kuonyesha Upendo na namna Mahakama hiyo inavyowathamini watoto hao.
Ameongeza
kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa msaada huo kwa lengo la kujenga
mahusiano mema baina yake na watoto hao ili waendelee kuipenda na kuwa
na mtazamo chanya juu ya utendaji wake.
‘
Nimekuja kukabidhi msaada huu kwa niaba ya Mahakama Kuu ya Tanzania kwa
Mahabusu hii ya Watoto ikiwa ni zawadi yao ya mwaka mpya, lengo letu ni
kujenga mahusiano mema kati yetu Mahakama na watoto hawa wajue kuwa
tunasaidia jamii katika masuala mbalimbali’’ Amesema Bw. Ndimbe.
Kwa
upande wake Afisa Mfawidhi wa Mahabusu hiyo Bw. Ramadhan Yahaya
akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ameishukuru Mahakama Kuu ya
Tanzania kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka Mahabusu hao.
Amesema
kitendo cha Mahakama Kuu ya Tanzania kuwapatia msaada huo kimewapa
faraja watoto hao na kuwafanya wajione wanathaminiwa na kupendwa na
Mahakama hiyo.
Ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mengine kuiga mfano huo ulioonyeshwa na Mahakama Kuu ya Tanzania ili kudumisha upendo miongoni mwa makundi ya watu wenye mahitaji maalum.
No comments:
Post a Comment